Friday, December 1, 2017

ALICHOKISEMA NYALANDU KUHUSU BIASHARA YA UTUMWA INAYOENDELEA NCHINI LIBYA

Aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii na Mbunge wa wa Singida Kaskazini aliyejiuzulu, Lazaro Nyalandu ameutaka Umoja wa Mataifa kuchukua hatua zaidi juu ya kinachoendelea nchini Libya.
Tokeo la picha la nyarandu
Amesema kuwa ni lazima hatua zichukuliwe kwa kile kinachoendelea nchini Libya ili kuweza kukomesha kile ambacho kinaendelea kwa sasa dhidi ya binadamu.

“Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika lazima uchukue hatua dhidi ya Libya sasa. tunachoshuhudia ni matusi kwa wanadamu,”amesema Nyalandu

Aidha, siku za hivi karibuni kumekuwa na taarifa zikiripotiwa kutoka Libya kuwa kumekuwa na biashara ya utumwa ikifanyika ikihusisha Libya kuuza Waafrika nchi za Ulaya.

Ubalozi wa Libya nchini Tanzani umesema kuwa Waafrika wanaodaiwa kuuzwa kutoka nchi hiyo, yawezekana walikuwa wanakabidhiwa kwa watoroshaji ili wawapeleke Ulaya na sio kuwauza kama watumwa.

No comments: