MSTAHIKI Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita amekutana na kufanya mazungumzo na ujumbe wa watu 10 kutoka Kisiwa cha Mayotte kilichopo Nchini Ufaransa.
Ujumbe huo ulikuwa umeambatana na wabunge watatu kutoka Nchini humo, Rais wa Shirikisho la wafanyabiashara wa Mayotte pamoja na wajumbe wengine ambao ni wawakilishi kutoka kampuni mbalimbali kisiwani humo.
Katika mazungumzo hayo, Mstahiki Meya Mwita na wageni wake wamejadili mambo mbalimbali ya maendeleo jijini hapa hususani masuala ya kibiashara ambapo amewakaribisha na kuahidi ushirikiano kwao.
Aidha Meya Mwita pia ameshangaa kuona ugeni huo kutoka Kisiwa cha Mayotte wakizungumza Kiswahili jambo ambalo alidai kuwa ni la kihistoria kutokana na historia ya Nchi hiyo.
Kutokana mshangao huo, ambao uliambatana na furaha ndani yake, aliwakabidhi zawadi ya Kamusi ya Kiswahili kwa lengo la kuendelea kujifunza zaidi Lugha ya Kiswahili pindi watakaporejea nchini kwao.
“ Nimefarijika na kushangaa baada ya kusikia asilimia 40 ya wananchi wakisiwa cha Mayote wanazungumza lugha ya Kiswahili, hii ni ajabu, lakini inaonyesha ninamna gani ambavyo watu wanaipenda Lugha yetu” amesema Meya Mwita.
Awali jumbe huo ulikutana na kufanya mazungumzo na Shirikisho la wafanyabiashara wenye Viwanda na Kilimo Tanzania.
Imetolewa leo Desemba 1 na Christina Mwagala, Afisa habari Ofisi ya Meya wa jiji.
Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Saalam Isaya Mwita akimkabidhi Rais wa Shirikisho la wafanyabishara na Viwanda wa Mayotte Hamidani Magoma Kamusi ya Kiswahili baada ya kuzungumza Kiswahili. |
No comments:
Post a Comment