Ikiwa leo
Tanzania imeadhimisha miaka 54 ya mapinduzi ya Zanzibar ,serikali Mkoani Geita
imetumia siku hiyo kwa kushirikiana na wananchi
wa Mulanda Kata ya Buseresere kufanya shughuli za maendeleo za ujenzi wa
shule ya sekondari kijijini hapo.
Ujenzi huo
ambao umeasisiwa na Mkuu wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi kwa kushirikiana na wanakijiji wa kijiji
hicho umetokana na adha ambazo wamekuwa wakizipata wanafunzi ambao wanasoma
shule ya sekondari ya Buseresere ambao wamekuwa wakitembea umbali wa kilomita
sita kufuata elimu.
Akizungumza
kwa niaba ya wananchi Diwani wa Kata ya
Buseresere,Godfrey Miti ,alisema maamuzi hayo ambayo yalichukuliwa na wananchi
yametokana na kwamba kata hiyo inawananchi wengi na kwamba shule iliyopo
ilikuwa haitosho kutokana na kwamba wanafunzi wa kidato cha kwanza 736 ambao wanatarajia kusoma kwenye shule ya
kata hali ambayo inaonesha kuwepo kwa wanafunzi wengi zaidi na kwamba
kukamilika kwa shule hiyo itasaidia kupunguza wingi wa wanafunzi kwenye shule
ya sekondari Buseresere.
Aidha kwa
upande wake mgeni rasmi kwenye
maadhimisho hayo ,ambaye ni mkuu wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi,aliwataka
wananchi kutambua kuwa akuna mgeni ambaye anaweza kuleta maendeleo na kwamba
maendeleo yanaitaji kuwa na mapinduzi ya kifikila huku akiwashukuru wananchi
kujitoa kwenye ujenzi wa shule hiyo.
Mhandisi,Luhumbi
ameongezea kuwa matarajio ni kuona
ifikapo mwishoni mwa mwaka 2018 kila kijiji kinakuwa na zahahati ili kuhepukana
na usumbufu wa wananchi kutembea umbali mrefu kufuata huduma za afya.
Maadhimisho ya
miaka 54 ya mapinduzi ya Zanzibar,
mapinduzi yaliyoshuhudia kuangushwa kwa utawala wa Sultan na familia yake
January 12 mwaka 1964.
Mwaka huu yamefanyika huku Serikali ya
mapinduzi ya Zanzibar ikiwa imepiga hatua katika kupambana na umasikini na
kuimarisha demokrasia licha ya changamoto kadhaa za kisiasa zinazoendelea
kushuhudiwa.
Wazanzibari
wanaona siku hii inapaswa kutumiwa na Serikali kujitathmini kuangalia hatua
walizopiga na changamoto ambazo zinaendelea kuikabili Zanzibar.
Zaidi ya
wanamapinduzi 800 walishiriki kwenye mapinduzi hayo yaliyoifanya Zanzibar kuwa
huru kutoka kwa utawala wa Kisultani.
Sherehe za
leo zimejumuisha vikosi vya ulinzi na usalama sambamba na maandamano ya
wananchi wa mikoa mitano ya Zanzibar.
No comments:
Post a Comment