Wednesday, March 21, 2018

DC WA NYAMAGANA ATOA ONYO KALI KWA WASAFIRISHAJI ABIRIA NA MIZIGO KIHORELA

Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mhe.Marry Tesha ametoa muda mwezi mmoja kwa wasafirishaji wa abiria na mizigo kwa kutumia tax, Kirikuu, Bajaji pamoja na Bodaboda ambao hawajasajiliwa, kuhakikisha wanasajiliwa ili kufanya shughuli hiyo kwa mujibu wa sheria.
Mhe.Tesha ameyasema hayo hii leo wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake ambapo ametoa muda hadi tarehe 20.04.2018 kwa wasafirishaji bubu wa abiria na mizigo (ambao hawajasajiliwa) kuhakikisha wanasajiliwa na kuanza kulipa kodi/ ushuru ambapo pikipiki za miguu mitatu na kirikuu ni shilingi elfu tano kwa mwaka na tax shilingi elfu kumi kwa mwaka.
Mbali na hayo pia Mhe.Tesha amezungumzia ratiba yake ya kutembelea Kata zote 18 za wilaya ya Nyamagana, kusikiliza kero za wananchi kuhusu migogoro ya adhri ambapo ratiba hiyo ilianza tarehe 13.03.2018 na itafikia tamati tarehe 25.04.2018
BMG Habari-Pamoja Daima!

No comments: