Wednesday, March 21, 2018

WATUHUMIWA 58 WAKAMATWA SAKATA LA DAWA ZA KULEVYA



zipo taarifa kuwa baadhi ya wananchi Mkoa wa Mjini Magharibi wanatumia, wanashiriki, wanafadhili au kusaidia biashara ya madawa ya kulevya kama ilivyo kwenye maeneo mengine nchini. 

Hata hivyo Serikali ipo kwenye vita kali ya kupambana na mtandao wa madawa ya kulevya na Inspekta Jenerali wa Polisi kwa kushirikiana na Kamisheni ya Polisi Zanzibar waliunda timu kutoka Kitengo cha Operesheni Maalum za Polisi Makao Makuu Dar es salaam kuja kuongeza nguvu katika ufuatiliaji wa kero hii kama ilivyo kwenye maeneo mengine ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

katika oparation hiyo kumeweza kubaini taarifa na kuwakamata watu kadhaa wanaohusika kwa namna moja au nyingine kwa kutumia, kuuza, kufadhili au kusaidia na mpaka sasa jumla ya watuhumiwa 105 wamekamatwa.

Na katika hao watuhumiwa walioshikiliwa waliopatikana na hatia ni 58 ambao kati ya hao watuhumiwa 26 wamefikishwa mahakamani tayari, na watuhumiwa 16 bado wako chini ya upelelezi na 16 wengine wapo chini ya uangalizi wa polisi(police supervisee.

Na vielelezo vilivyopatikana ni Heroin kete 1293 na vifuko vitatu ambavyo ni sawa na gramu 74.385 na banghi vifurushi 373 na nyingine vifuko vitatu.

Wito kwa wananchi wote

Tahadhari kwa wananchi wote wanaohusika kwenye mtandao huu kuacha mara moja kwa kuwa vita hii imeshaanza na inaendelea kwa lengo la kuhakikisha usalama wa vizazi vilivyopo na vizazi vijavyo maana madawa haya yanaathiri zaidi vijana ambao ndiyo muhimili na nguvu kazi ya Taifa.


Aidha nawapongeza wananchi wote waliotoa ushirikiano wa kutoa 
taarifa za uhalifu huu bila ya kuona muhali. Niwaombe wananchi wote
kuendelea na ushirikiano huu wa kutoa taarifa.

Mwisho natuma salamu kwa watuhumiwa wote waliotoroka kule 
walipo wajue kuwa wanatafutwa na watakamatwa ili wahojiwe na
hatimae kufikishwa Mahakamani.


Liberatus Sabas – DCP
Mkuu Wa Uperesheni Maalum za Polisi Tanzania
21.03.2018

No comments: