Monday, March 26, 2018

MAALIM SEIF ALIPONGEZA BARAZA LA MAASKOFU KWA WARAKA WAO

KATIBU Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad amelipongeza Baraza la Maaskofu la Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) kwa kutoa waraka mzito wa ujumbe wa Sikukuu ya Pasaka.
 Tokeo la picha la maalim seif leo
Waraka huo ulitolewa mwishoni wa wiki iliyopita ambao mbali na kuzungumzia masuala ya kiroho, umetaja changamoto tatu na kuzifikisha kwa waumini wake “ili ziongeze mzigo wa kuliombea taifa letu na viongozi wake.”

Changamoto zilizotajwa katika waraka huo uliopewa jina la “Taifa Letu Amani Yetu” na kusainiwa na maaskofu 27 wa kanisa hilo nchini ni hali ya kijamii na kiuchumi, maisha ya siasa na masuala mtambuka likiwamo suala la Katiba Mpya.

Akizungumza leo Machi 26, 2018 jijini Dar es salaam wakati akisoma maazimio manne ya Kamati ya Utendaji ya Taifa ya chama hicho iliyokutana leo, Maalim Seif amesema anafarijika kuona  viongozi wa dini  wanakemea mambo ambayo hayaendi sawa nchini.

“Nimefarijika kuona viongozi wa taasisi za dini wakizungumza pale ambao wanaona mambo hayaendi sawa. Tusitafsiri  kwamba wanafanya siasa, hapana ni haki yao kukemea, ” amesema Maalim Seif.
Amesema angetamani kuona viongozi wengine wa dini  wakionyesha misimamo kama maaskofu hao.

Aidha, Maalim seif amemponda Mwenyekiti wa Chama hicho, Prof. Ibrahim Lipumba kwa kitendo cha kuwavua uanachama wanachama nane na kupoteza sifa za kuwa wabunge jambo ambalo wamepambana hadi kurudishiwa uanachama baada ya kudai haki yao mahakamani.

Maalim amesema kwa sasa wanafanya jitihada za kisheria ili kuwarudisha wabunge hao Bungeni wakati kesi yao ya msingi ikiwa inaendelea mahakamani.

No comments: