Thursday, March 22, 2018

TIGO NA TTCL WAUNGANA PAMOJA KUFANYA MIAMALA YA PESA KWA WATEJA WAO


     
Afisa Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Fedha Tigo, Hussein Sayed (kushoto) akipeana mkono wa pongezi na Mkuu wa Idara ya TTCL Pesa, Moses Alphonce mara baada ya makubaliano ya matumizi ya huduma za miamala ya makampuni hayo itakayowezesha mtumiaji kuingiza pesa moja kwa moja kwenye akaunti ya mtumiaji kwa gharama nafuu, hafla iliyofanyika jijini Dar Es Salaam leo.
Shirika kubwa zaidi la kitanzania la mawasiano ya simu, na watoa huduma ya simu zisizohamishika, broadband, bidhaa na huduma za internet wanaoongoza Tanzania pamoja kampuni ya maisha ya kidigitali inayoongoza Tanzania, Tigo. Leo wameingia katika ubia mkubwa, ambapo wateja kutoka katika taasisi hizi mbili wataweza kutuma na kupokea fedha kati ya mitandao hiyo miwili moja kwa moja katika akaunti zao.

Akiongea wakati wa kutangaza ubia huo katika ukumbi wa Golden Jubilee Towers Jijini Dar es salaam, Mkuu wa Idara ya Huduma za Fedha kwa njia ya simu za mkononi  wa TTCL, Moses Alphonce amesema kwamba, “Tunafuraha sana kutia sahihi makubaliano ya ushirikiano huu ambao unaenda kuwanufaisha wateja wetu na wananchi wote kwa ujumla. Ujio wa TTCL PESA katika sekta hii ya mawasiliano ina lengo la kutengeneza ushirikishwaji wa masuluhisho ya kifedha kwa watanzania wote. Lengo letu ni kubadilisha mahitaji ya kila siku ya kifedha ya watu wetu yawe yasiyo ya fedha tasilimu na kuwa wawezeshaji wa miamala yote ya kidigitali inayofanyika Tanzania”.

Aliongezea kuwa, tuna mifumo bora sana ambayo inaweza kutoa uwezo kwa makampuni na taasisi za kiserikali uwezo wa kutoa malipo ya kidigitali kwa mamilioni ya watanzania.  

TTCL PESA inatoa huduma ya kifedha ya kidigitali ambayo ni bei nafuu, ya haraka na salama ambayo inazidi huduma za benki kupitia simu za mkononi, huduma za malipo, kuongeza muda wa maongezi na uhamishaji wa fedha.

Kwa upande wake, Afisa mkuu wa Huduma za kifedha za simu za mkononi wa Tigo, Hussein Sayed amesema kwamba makubaliano  haya kuwa ni mwanzo wa ushirikiano mkubwa lakini pia jukumu la uanzilishi la Tigo katika huduma za fedha kupitia simu za mkononi, ushirikiano tayari umeshasainiwa. Jambo hili limeziakikishia kampuni hizi mbili zenye shauku ya kuwapatia wateja wao huduma ya kiwango cha juu katika zama hizi za huduma za kifedha za kidigitali. “Kwa makubaliano haya kwa mara nyingine tena tunaisaidia Tanzania kuimarisha jukumu lake lisiliokwepeka katika waanzailishi wa ushirikishwaji wa kifedha kwa njia za kidigitali duniani. Ushirikiano mara zote huwa ni chachu ya ukuaji katika sekta ya fedha kwa njia za simu za mkononi.” Alisema Sayed.

“Tumetambulisha sokoni idadi kadhaa ya bidhaa zenye ubunifu na tuna nia ya kupanua watumiaji wetu kwa kushirikiana na watoa huduma wenzetu walioko sokoni” Aliongeza Hussein.

Katika mwezi June 2014, Tigo iliibuka kuwa ya kwanza baada ya kufanikiwa kuzindua makubaliano ya ushirikiano ya kwanza ya aina yake ambayo yanawawezesha mamilioni ya wateja wa Tigo Pesa kutuma fedha na kupokea fedha kwa watoa huduma wengine waliosajiliwa. 

No comments: