Saturday, April 14, 2018

QNET: Kusaidia Maendeleo ya Michezo Afrika

Na Mwandishi Wetu

Sekta ya michezo barani Afrika inakua kwa kasi sana. Iwe katika michezo ya riadha (ambayo Afrika ya Mashariki na pembe ya Afrika huwa wanaongoza katika bara zima na hata katika mashindano ya kiulimwengu kwa ujumla), au michezo mingine. Bara la Afrika linabadilika taratibu kuwa mabingwa katika shughuli mbalimbali za michezo ambayo mpaka hivi karibuni zimetawaliwa na nchi za ulaya na Asia.

Kwa ujumla katika mchezo wa mpira wa miguu Afrika imeonyesha viwango vikubwa kwa timu za kiafrika kufanya vizuri katika mashindano ya kidunia. Tunashukuru umaarufu wa mchezo wa mpira wa miguu miongoni mwa mashabiki ndani ya Afrika na wadhamini wapya wenye mapenzi mema wanaojitokeza, wapenzi wa michezo na wadau mwengine.

Miongoni mwa wale ambao wameingia katika ushirika na vyama vikubwa vitatu vya mpira wa miguu barani Afrika ni QNET, kampuni ya mauzo ya moja kwa moja yenye asili ya Asia ambayo biashara yake iko Afrika na ambayo kwa hakika dunia nzima inaichukulia kuwa ni miongoni mwa mashirika makubwa katika tasnia hiyo.

Mapema mwaka huu, QNET ilisaini mkataba wa ushirikiano wa muda wa miaka miwili na mabingwa wa ligi za vilabu vya Afrika: Ligi ya Mabingwa CAF, Ligi ya Kombe la Shirikisho na  Ligi ya Kombe la Super Cup katika mpango wa udhamini unaolenga katika wigo mpana wa kidigitali na shughuli ambazo zinalenga kukuza ushirikiano wa mashabiki na wawakilishi wa QNEt (IRs) Afrika.

Akizungumzia kuhusu udhamini huo, CEO wa QNET bwana Trevor Kuna alisema kwamba ushirikiano huo na CAF ni uwekezaji muhimu sana kwa kampuni, ambayo unaendana na wateja wake na jamii ya Afrika kwa ujumla. Ikiwa inawianisha bidii za kimichezo na biashara ya QNET. Bwana Kuna alihamasisha: “Kama mpira wa miguu, QNET inaunganisha dunia na kuhamaisha ari ya kufanya kazi kwa pamoja kama timu miongoni mwa wawakilishi wake (IRS) na kila mmoja anayehusika katika biashara yetu. Kufanya kazi kama timu na utendaji thabini ni mambo ambayo yako sambamba katika mpira wa miguu na biashara ya masoko ya mtandao” 

Udhamini huu pia ni kilemba kingine katika kofia ya QNET na inaonyesha tena jitihada za kampuni ya mauzo ya moja kwa moja katika kuthamini maadili ya michezo: Umakini, kufanya kazi kwa bidii na kuongeza bidii mpaka kiwango cha mwisho. Ushirikiano huu unakuja kama jukumu la QNET kama mshirika rasmi wa mauzo ya moja kwa moja wa Klabu ya Mpira wa Miguu wa Manchester City, shughuli ambayo imeiwezesha QNET kuunganisha msisimko wa mpira wa miguu na shauku ya mashabiki katika msisimko wa mauzo ya moja kwa moja na msukumo wa wawakilishi (IRs) wa QNET

Aliongeza kwamba ushirikiano wa kampuni hii na CAF umepelekewa zaidi na shauku ya kampuni hii kutengeneza fursa za ushiriki ikiwa inalenga mashabiki wa mchezo wa mpira wa miguu katika bara la Afrika pamoja na kuandaa matamasha ya kuangalia mechi kwaajili ya wasambazaji na IRs katika nchi mbalimbali barani Afrika.  

Ushirikiano huu pia ni ushahidi wa kuuzika kwa mchezo wa mpira wa miguu wa Afrika kama bidhaa – jambo ambalo limehamasisha makampuni ya kiwango cha kimataifa kama QNET kuonyesha nembo yao katika mchezo ambao unatazamwa zaidi duniani.

QNET ina maono bora ya kibiashara katika bara la Afrika ambayo ina endesha shughuli zake katika maeneo ya Afrika ya Magharibi na Afrika ya Mashariki ambako kampuni ya mauzo ya moja kwa moja imetoa fursa za ujasiriamali kwa maelfu ya watu kupitia bidhaa zake zinazoweza kubadilisha maisha zinazotolewa kupitia mfumo wao wa biashara ya mtandao (e-commerce) kwenda kwa wateja na IRs.

Bidhaa za kampuni zinajumuisha pamoja na bidhaa za huduma binafsi, bidhaa za majumbani, saa, vito, safari za mapumziko, elimu na zingine nyingi – ambazo zinauzwa kupitia ofisi za QNET na mawakala wao walioko duniani kote, pia kutoka kwa waendeshaji walioko ndani ya maeneo tofauti katika nchi mbalimbali.

QNET ambayo inasherehekea kutimiza miaka 20 mwaka huu, na ambayo inajigamba kwa kukua kwake kutoka kuwa kampuni ndogo yenye bidhaa moja kwenda kuwa kampuni yenye zaidi ya bidhaa 100 za aina mbalimbali tofauti, inabakia kuwa imejidhatiti kutoa programu za mafunzo ya mara kwa mara, kuhamasisha mwenendo imara wa maadili ya utendaji, kuwasaidia wasambazaji wake kwa kuwapatia vifaa vya matangazo na vifaa vya kufanyia biashara na kuendelea kutafuta au kutengeneza bidhaa sahihi kwaajili ya  wateja wao walioko dunia nzima.


No comments: