Friday, August 19, 2022

NSSF yajipanga kukusanya Trioni 7.3 katika Mwaka wa fedha 2022/2023

Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) umepanga kukusanya kiasi Cha shilingi trioni 7.3 katika Mwaka wa fedha 2022 / 2023 Kutoka katika vyanzo vyake mbalimbali.

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Bw. Masha Mshomba akiongea na Waandishi wa habari mapema leo jijini Dar es salaam.

Kauli hiyo imetolewa leo Agosti, 19 jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa huo Bw. Masha Mshomba, alipokua akizungumza na waandishi wa habari, akitoa Taarifa ya Utendaji wa Mfuko pamoja na Vipaumbele vya Mfuko kwa mwaka wa Fedha  2022/23.

Amesema kuwa, ukuaji huo ni mkubwa tofauti na miaka miwili ya nyuma iliyopita ambapo thamani ya Mfuko ilikuwa ni Shilingi Trilioni 4.3 na kuwa ukuaji huo umechangiwa na ongezeko la makusanyo ya michango.

"Tumepata mafanikio makubwa katika suala zima la ukuaji wa Mfuko na hii imesababishwa na sababu kadhaa ikiwemo kuweka misingi imara na madhubuti ya ukusanyaji wa mapato" amesema Mshomba.

Ameongeza kuwa, katika mwaka wa fedha ulioishia tarehe 30 Juni, 2022, Mfuko ulikusanya zaidi ya Shilingi Trilioni 1.42 kwamba makusanyo hayo ni zaidi ya hata bajeti ambayo walijipangia iliyokuwa Shilingi Trilioni 1.38, ambapo pia Mfuko umeboreshaji sana udhibiti wa matumizi jambo ambalo limechangia ukuaji wa NSSF.

Amesema kuwa, mafanikio mengine yaliyopatikana, ni pamoja na uboreshaji wa huduma hasa kwa kutumia mifumo mbalimai ya TEHAMA ambapo sasa mwanachama na wadau wanaweza kupata huduma popote walipo bila ya kufika katika ofisi za NSSF kwa kutumia mifumo ya waajiri na wanachama yaani Employer Potal na Member Potal.

Mshomba alisema Mfuko pia unapata matokeo mazuri sana katika Uwekezaji hasa ukizingatia kuwa wanawekeza katika maeneo salama ambapo katika kipindi cha miaka miwili uwekezaji umeleta mapato makubwa.

"Ilikuwa haijafikiwa NSSF kuweza kupata mapato ya mwaka zaidi ya Shilingi bilioni 500 lakini katika mwaka huu wa fedha umepata zaidi ya Shilingi bilioni 600,matokeo haya ya uwekezaji yametokana na Mfuko kujikita zaidi katika uwekezaji kwenye maeneo ambayo yanaleta faida kwa Mfuko na kuhakikisha wanaudhibiti wa fedha"amesema Mshomba.

Hata hivyo, amesema chachu kubwa ya mafanikio ya NSSF imechagizwa na kasi ya utendaji wa Rais Samia Suluhu Hassan kwa sababu amekuwa chachu ya ongezeko kubwa la wawekezaji hapa nchini hususan katika sekta binafsi kutokana na kufungua fursa za uwekezaji.

Kuhusu waajiri kutowasilisha michango alisema wameweka mikakati mbalimbali kwa kushirikiana na taasisi nyingine za Serikali ili kupata orodha kamili ya waajiri ambao watawafikia na kufuatilia michango ya wanachama.

Mshomba aliwahamasisha Watanzania wote kushiriki katika zoezi zima la Sensa ya Watu na Makazi ifikapo tarehe 23 Agosti, 2022 ili waweze kuhesabiwa.

No comments: