Wednesday, November 29, 2017

JUMUIYA YA WAZAZI MKOA WA GEITA YACHAGUA MWENYEKITI MPYA

Wajumumbe wa Jumuiya ya wazazi wakiwa kwenye mstaari kwaajili ya kupiga kura wa kumchagua mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi wa mkoa wa Geita na wajumbe.

Mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi Mkoa wa Geita ambaye amemaliza muda wake,Doto Biteko akiwashukuru wajumbe kwa ushirikiano ambao walimpatia wakati wa uongozi wake.

Baadhi ya wagombea kwenye nafasi mbali mbali ndani ya jumuiya hiyo.

Wasimamizi wa uchaguzi  wakitambulishwa kabla ya zoezi kuanza.

Mkuu wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi akijitambulisha mbele ya wajumbe wa mkutano huo.


Mwenyekiti aliyechaguliwa kwenye jumuiya ya wazazi wa chama cha mapinduzi Mkoani Geita,Bw Lucas Singu Mazinzi  akiwashukuru wajumbe ambao wamemchagua.

Msimamizi wa uchaguzi   ambaye  ni Katibu wa CCM Mkoa wa Simiyu Donald Magesa  akielekeza namna ambavyo wanatakiwa wajumbe kupiga kura.

Daud Katwale Ntinonu akijitambulisha na kuelezea namna ambavyo ameamua kurudi ndani ya chama ca mapinduzi akitokea chama cha CHADEMA.

Katibu wa jumuiya ya wazazi Mkoani Geita,Joseph Mwita akielezea namna ambavyo zoezi la uchaguzi lilivyofanyika(Picha na Joel Maduka)
Na,Consolata Evarist,Geita


Jumuiya ya umoja wa wazazi wa chama cha mapinduzi(CCM) Mkoa wa Geita  imefanya  uchaguzi wa mwenyekiti na wajumbe wa mkutano Mkuu ambapo katika uchaguzi huo,Bw Lucas Singu Mazinzi aliibuka mshindi kwa kupigiwa kura 250.


Akitangaza matokeo katika uchaguzi wa kumchagua mwenyekiti mpya wa jumuiya hiyo    ,msimamizi wa uchaguzi   ambaye  ni Katibu wa CCM Mkoa wa Simiyu Donald Magesa  , alisema kura ambazo zilipigwa ni 320  na ambazo ziliharibika ni 19  kura harari 301.

 Alisema kuwa   ,Lucas Singu   ameshinda dhidi ya wagombea wenzake   Hewa Samweli Masatu  aliyepata kura 36 na Mayengo Simion Kitindi ambaye alipata kura 15.

Aidha Magesa aliendelea  kutaja  nafasi za   wajumbe watakaowakilisha mkutano mkuu Taifa kutoka kwenye jumuiya hiyo, kuwa ni Ibrahimu Jumu Ibrahimu   Kura 38 , John Kafimbi Saulo kura 11, Charles Kazungu Mabeyo kura 192 na Rose Venasi Mweko  55.


Awali mbunge wa jimbo la Bukombe ambaye amemaliza nafasi yake ya uenyekiti wa jumuiya hiyo Doto Biteko,alisema   ndani ya kipindi chake cha uongozi amejidhatiti katika kuleta maendeleo ndani ya jumuiya hiyo ikiwa ni pamoja na kuwa na miradi ambayo ni endelevu mfano uwanja ambao upo kwenye Wilaya ya Bukombe ambacho kinatarajia kujengwa chuo na kusimamia shughuli zote za maeneo ya uchimbaji madini ya dhahabu yanayomilikiwa na jumuiya hiyo.

Aliongeza kuwa anaamini ambaye amechaguliwa kurithi kiti chake hataweza kusaidia kwa kiasi kikubwa kukamilisha pale ambapo ameishia.

Aidha Mwenyekiti wa  jumuiya hiyo ambaye amechaguliwa,Bw  Singu mbali na kuwashukuru wajumbe ambao wamempatia ushindi huo ,alisema mikakati aliyonayo ni kutafuta miradi mikubwa zaidi ndani ya jumuiya ikiwa ni pamoja na kukisaidia chama hicho kutimiza malengo yao.

Pia amewashukuru Wagombea wenzake ambao alikuwa akichuwana nao kwenye kinyanganyiro hicho kwa kukubaliana na matokeo ambayo yametangazwa.

Tuesday, November 28, 2017

Tigo Yatangaza Dili ya Kipekee ya Simu za Smartphone

Mkuu wa Bidhaa na Huduma wa Tigo, David Umoh akizungumza na waandishi wa habari   (hawapo pichani) mapema leo kuhusu ofa mpya ya 'Simu Janja kwa Mpango' kutoka Tigo katika msimu huu wa sikukuku. Wateja wa Tigo wana fursa  ya kupata simu za smartphone bure kwa njia rahisi kupitia menu mpya ya *147*00# kwa kununua bando au kwa kulipia kidogo kidogo. Kushoto ni Meneja mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael. 



Meneja mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael akifafanua jambo kwa waandishi wa habari jana kuhusu ofa mpya ya 'Simu Janja kwa Mpango' kutoka Tigo katika msimu huu wa sikukuku. Wateja wa Tigo wana fursa  ya kupata simu za smartphone bure kwa njia rahisi kupitia menu mpya ya *147*00# kwa kununua bando au kwa kulipia kidogo kidogo.Kulia ni Mkuu wa Bidhaa na Huduma wa Tigo, David Umoh.

Pata Simu za Smartphone BURE kutoka Tigo katika msimu huu wa sikukuuu!


Dar es Salaam, Novemba 28, 2017- Kampuni inayoongoza kwa mageuzi ya kidigitali, Tigo Tanzania, leo imetangaza dili za kipekee zinazohusu simu za Smartphone ambazo zitahakikisha kila mtu anakuwa sehemu ya maisha ya kidigitali katika msimu huu wa Krismasi na mwaka mpya.

Akitangaza ofa hizo za msimu wa sikukuu Dar es Salaam leo, Mkuu wa Bidhaa na Huduma wa Tigo, David Umoh alisema dili hizo kemkem zinapatikana kwa kupiga namba ya menu mpya *147*00#  na kubonyeza kitufe cha ‘Duka la Simu’ ili kuchagua simu unayoipenda, na kisha kutembelea Duka lolote la Tigo nchi nzima ili kuchukua simu uliyoichagua.

‘Katika ofa ya kwanza, wateja wa Tigo wanaweza kupata simu ya Smartphone BURE kirahisi kwa kununua bando kuanzia TZS 25 000 ambayo - pamoja na Smartphone ya bure – inawapa 1GB data, SMS 50 na dakika 50 za kupiga Tigo – Tigo,’ alisema.

Katika dili ya pili, wateja wa Tigo pia wanaweza kupata Smartphone kwa kuchagua mpango wa kulipia kwa miezi sita. Ofa hii inawahusu wateja wa sasa wa Tigo ambao wanakidhi vigezo vilivyowekwa.

Katika msimu huu wa sikukuu, Tigo pia inatoa ofa ya ‘Lipia sasa, Chukua Baadaye’ ambapo wateja wanaruhusiwa kuchagua simu yoyote ile wanayoipenda na kisha kufanya malipo ya awamu kila mwezi, ambapo wataruhusiwa kuchukua simu waliyoichagua baada ya kumaliza mpango wa malipo ya kila mwezi.

‘Kupitia ofa hizi kabambe, Tigo inaendelea kushika hatamu za ubunifu unaoendana na mahitaji ya wateja kwa kuwezesha kila mtu kumiliki mojawapo ya hizi simu bomba za Smartphone, ambazo zimeunganisha na mitandao ya jamii. Hii ndio njia yetu ya kuhakikisha kuwa kila mtu anakuwa sehemu ya maisha na mabadiliko ya kidigitali yanayoongozwa na Tigo,’ David alisema.

‘Tunawakaribisha wateja wetu wachangamkie ofa hizi za kipekee katika msimu huu wa sikukuu kwa kujigiftisha au kuwagiftisha ndugu, jamaa na marafiki kwa simu hizi bora za smartphone. Simu zote zinakuja na mpango rahisi wa malipo, bando murwa na ofa za kipekee ambazo zitahakikisha kila mtu ataweza kufurahia na kutunza kumbukumbu za shamrashamra za sikukuu katika simu yake mpya ya smartphone kutoka Tigo.’

Jumanne ya Kutoa-Zaidi ya Million 20 zapatikana Kusaidia watoto wenye matatizo ya Vichwa vikubwa na Mgongo wazi

Zaidi ya milioni 20 zimetolewa na wananchi pamoja na Taasisi mbalimbali hapa  nchini ikiwa ni mchango wa kusaidia matibabu na kununua vifaa tiba kwa ajili ya  watoto wenye vichwa vikubwa na migongo wazi.
Ikiwa Jana ni Jumanne ya kutoa (GIVING TUESDAY) kote duniani na Taasisi ya Foundation for Civil Society iliadhimisha kwa kuwasaidia watoto hawa kwa kuwapatia vitu hivyo,huku kauli mbiu ya mwaka huu ikiwa ni changia, okoa maisha.

Akikabidhi misaada hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Foundation For Civil Society Bw. Francis Kiwanga alisema kuwa wafanya kazi wa Taasisi hiyo huwa wanatenga asilimia moja kwa kila mtumishi katika mshahara wake kwa ajili ya kurudisha fadhila na asante kwa jamii.
Aliendelea kwa kusema kuwa wao kama waanzilishi wa kampeni hiyo walichanga na kufikisha million sita, ila michango mingi ilitoka kwa wananchi na taasisi zilizoguswa na tatizo hilo hivyo kuona haja ya kuwasaidia watoto hao.

Aidha mkurugenzi huyo alisema kuwa msaada huo utalenga watoto 100 waliopo katika camp hizo kwa kufanyiwa upasuaji na mambo mengine madogo madogo yatakayohitajika katika zoezi hilo.

Lakini pia taasisi ya Foundation For Civil Society ikishirikiana na wadau wake wameweza kutoa kadi za bima ya afya za NHIF 100 ambazo zimegharimu kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 5 kuwasaidia watoto hao kwa matibabu hayo na mengineyo.

Aidha Mkurugenzi huyo aliwasihi  watanzania kujitolea kuwasaidia wenzetu ambao hawajiwezi na wanaohitaji michango yetu kwani kutoa ni moyo na kadiri unavyotoa ndivyo unavyobadirikiwa.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa kitengo cha mifupa MOI Dr. Respicious Boniface alisema kuwa watoto hao wakipatiwa matibabu mapema wanaweza kuwa sawa kama watoto wengine, lakini kinachofanya wazazi washindwe ni gharama za matibabu.

Daktari huyo alisema kuwa changamoto nyingine inayowakabili wao kama wauguzi ni uchache wa vyumba vya upasuaji kwani vyumba vilivyopo havitoshi kwa kufanyia zoezi hilo ambapo amesema kuwa kwa siku wanawafanyia upasuaji zaidi ya wagonjwa 30.

Aidha Daktari huyo aliwapongeza shirika la  Foundation for Civil Society kwa kuamua kuwasaidia watoto hao ambao wanapata tabu kwa matatizo ya vichwa vikubwa na migongo wazi na asilimia kubwa wazazi wao hawana uwezo wa kumudu gharama za matibabu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Foundation for Civil Society Bw. Francis Kiwanga akizungumza katika maadhimisho ya Jumanne ya kutoa maarufu kama GIVING TUESDAY yaliyofanyika kitengo cha MOI Muhimbili Jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya Tiba ya Mifupa MOI Dr. Respicious Boniface akitoa neno la shukrani kwa wadau waliotoa msaada katika taasisi hiyo kwa kusaidia watoto wenye vichwa vikubwa na migongo wazi Katika Taasisi ya mifupa MOI Jijini Dar es salaam

Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya Tiba ya Mifupa MOI Dr. Respicious Boniface akimkabidhi zawadi ya cheti Mwenyekiti wa UN chapter UDSM Bi. Faith Lawrance Katika shughuuli hiyo.



Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya Tiba ya Mifupa MOI Dr. Respicious Boniface akimkabidhi zawadi ya cheti Bi. Adella January Msofe katika maadhimisho ya siku ya kutoa duniani maarufu kama GIVING TUESDAY Muhimbili Dar es salaam.

Mkurugenzi Mtendaji wa Foundation for Civil Society Bw. Francis Kiwanga akimkabidhi hundi ya shilingi milioni nane Mkurugenzi  Mtendaji wa taasisi ya Tiba ya Mifupa MOI Dr. Respicious Boniface kwa ajili ya matibabu ya watoto wenye vichwa vikubwa na migongo wazi.


Baadhi ya wazazi na wageni walioudhuria hafla hiyo ya kutolewa kwa msaada wa kusaidia matibabu kwa watoto wenye vichwa vikubwa na migongo wazi jijini Dar es salaam.




VIDEO-SAMIA SULUHU ALIVYOKUTANA NA LISSU LEO NAIROBI

MKURUGENZI MKUU MSD AFANYA ZIARA HOSPITALI JIJINI DAR ES SALAAM

 Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Laurean Bwanakunu (kushoto), akizungumza na viongozi mbalimbali wa Hospitali ya Sinza alipofanya  ziara ya kikazi katika Hospitali hiyo na  Mwananyamala jijini Dar es Salaam leo, ili kubaini changamoto zilizopo za  upatikanaji wa dawa na vifaa tiba na kuzipatia ufumbuzi wa pamoja. Kutoka kulia ni Meneja wa MSD Kanda ya Dar es Salaam, Celestine Haule na Mganga Mkuu wa Hospitali ya Sinza, Chrispin Kayola.
 Maofisa wa Hospitali ya Sinza wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Laurean Bwanakunu (hayupo pichani)
 Mkutano ukiendelea.
  Mganga Mkuu wa Hospitali ya Sinza, Chrispin Kayola, akizungumza katika mkutano huo.
 Laboratory Manager wa Hospitali ya Sinza, Emmanuel Kiponda, akichangia jambo kwenye mkutano huo.
 Meneja wa MSD Kanda ya Dar es Salaam, Celestine Haule, akizungumza kwenye mkutano huo.
 Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Laurean Bwanakunu, akiwa katika picha ya pamoja na maofisa wa Hospitali ya Sinza baada ya kufanya nao mazungumzo.
Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Laurean Bwanakunu, akiwa katika picha ya pamoja na maofisa mbalimbali wa Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala.


Na Dotto Mwaibale

MKURUGENZI Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Laurean Bwanakunu amewatembelea wateja wa MSD wanaohudumiwa na Kanda ya MSD Dar e's Salaam ukiwa ni pamoja na Hospitali ya Mwananyamala na Sinza kubaini changamoto zilizopo katika upatikanaji wa dawa na vifaa tiba ili kuzipatia ufumbuzi.

Katika ziara hiyo iliyofanyika jumanne jijini Dar es Salaam Bwanakunu amewataka wateja hao kufanya Maoteo ya mahitaji yao sahihi na kuyawasilisha Msd kwa wakati kwa mujibu wa sheria yaani tarehe 30 Januari kila mwaka,hasa dawa na vifaa tiba vinavyonunuliwa kwa Manunuzi maalumu.

Bwanakunu alihimiza watoa huduma katika hospitali hizo kutambua jukumu walilonalo katika usimamizi wa matumizi ya dawa na vifaa tiba kwa wananchi.

Akizungumza akiwa Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala Bwanakunu alisema anazitambua changamoto zilizopo za usambaji wa dawa na vifaa tiba na wamedata msaada wa magari kutoka Global Fund ambayo yataboresha usambazaji kutoka mara nne kwa mwaka hadi mara sita kwa mwaka.

Kuhusu vifaa vya Manunuzi maalumu Bwanakunu amesema hospitali zikiwa zinaomba kwa wakati mmoja ingerahisisha kuagiza vifaa hivyo mapema,badala ya kila hospitali kuleta kwa wakati wake.

"Vifaa hivi tunaagiza nje ya nchi na mchakato wake unachukua muda mrefu na changamoto kubwa " alisema Bwanakunu.

Mganga Mkuu wa Hospitali ya Sinza, Chrispin Kayola alisema hali ya upatikanaji wa dawa na vifaa tiba katika hospitali hiyo kwa sasa ni asilimia  80 .

"Changamoto iliyopo ni uhaba wa vitendanishi vya maabara na vifaa vya macho na meno ambavyo tunapata chini ya kiwango hivyo havikidhi mahitaji tuliyonayo," alisema.

Kwa upande wake Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala, Daniel Mkungu alisisitiza haja ya ushirikiano baina ya Hospitali hizo na MSD ili kuboresha huduma za afya hapa nchini.

Ziara hiyo ya mkurugenzi huyo itaendelea tena kesho katika baadhi ya hospitali zilizopo jijini Dar es Salaam.


MASAUNI, DK. MAKAKALA WAZUNGUMZA NA WAVUVI MKOANI MARA,WAWAASA KUSHIRIKIANA NA VYOMBO VYA ULINZI KUDHIBITI UHALIFU

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na wananchi wanaoishi na kufanya shughuli zao za uvuvi Ziwa Victoria, katika kijiji cha Nyang’ombe kilichopo wilayani Rorya, Mkoani Mara.Katika ziara hiyo Naibu Waziri aliambatana na Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dk. Anna Makakala ikiwa na lengo la udhibiti uhalifu na uingiaji wa kinyume na sheria kwa raia kutoka nchi jirani.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dk. Anna Makakala , akizungumza na wananchi wanaoishi na kufanya shughuli zao za uvuvi Ziwa Victoria  katika kijiji cha Nyang’ombe kilichopo wilayani Rorya, mkoani Mara. Lengo la ziara hiyo ni   kudhibiti uhalifu na kudhibiti uingiaji wa kinyume na sheria kwa raia kutoka nchi jirani.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

 Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima, akizungumza na wananchi wanaoishi na kufanya shughuli zao za uvuvi Ziwa Victoria katika kijiji cha Nyangombe, kilichopo wilayani Rorya, mkoani Mara. Lengo la ziara hiyo ni  kudhibiti uhalifu na kudhibiti uingiaji wa kinyume na sheria kwa raia kutoka nchi jirani.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

Mwananchi wa  kijiji cha Nyang’ombe akiuliza maswali kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni, wakati wa ziara ya kikazi ambapo naibu waziri aliongozana na Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dk. Anna Makakala, lengo la ziara hiyo ni kukagua  udhibiti uhalifu na  uingiaji wa kinyume na sheria kwa raia kutoka nchi jirani.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

Wananchi wakishangilia jambo wakati Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni (hayupo pichani), akizungumza  katika mkutano uliofanyika kijiji cha Nyang’ombe ,wilayani Rorya. Naibu Waziri yupo katika ziara ya kikazi ikiwa na lengo la kukagua  udhibiti uhalifu na  uingiaji wa kinyume na sheria kwa raia kutoka nchi jirani.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

Shirika la Kivulini lasaidia uanzishaji wa Kiwanda katika Shule ya Wasichana Bwiru Mwanza

Shule ya Wasichana Bwiru iliyopo Jijini Mwanza imezindua kiwanda cha mfano, fuatilia hafla ya uzinduzi huo ambayo imefanyika jana ikiwa ni sehemu ya "Maadhimisho ya Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia" ambayo huadhimishwa kila mwaka kuanzia Novemba 25 hadi Disemba 10.
Uzinduzi wa kiwanda kidogo katika shule ya wasichana ya kidato cha tano na sita Bwiru iliyopo Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza.[/caption] [caption id="attachment_29960" align="alignleft" width="620"] Mgeni rasmi, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt.Angeline Mabula akikagua bidhaa mbalimbali zinazotengenezwa shuleni hapo.[/caption] [caption id="attachment_29961" align="alignleft" width="620"] Mgeni rasmi akijionea picha mbalimbali zinazochorwa shuleni hapo.[/caption] [caption id="attachment_29962" align="alignleft" width="620"] Mgeni rasmi akijionea utengenezaji wa sabuni pamoja na dawa za chooni.[/caption] [caption id="attachment_29963" align="alignleft" width="620"] Mgeni Rasmi, Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt.Angeline Mabula akizungumza kwenye uzinduzi huo.[/caption] [caption id="attachment_29964" align="alignleft" width="620"] Mkuu wa shule ya wasichana Bwiru, Mwalimu Mackrida Shija akizungumza kwenye uzinduzi huo.[/caption] [caption id="attachment_29965" align="alignleft" width="620"] Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilemela, Renatus Mulunga akizungumza kwenye ufunguzi huo ambapo aliahidi ushirikiano katika kuendeleza kiwanda hicho.[/caption] [caption id="attachment_29966" align="alignleft" width="620"] Mwanafunzi wa shule ya wasichana Bwiru, Dorophy James (kushoto), akisoma risala ya ufunguzi. Kulia pia ni mwanafunzi wa shule hiyo Delvina Mollel.[/caption] [caption id="attachment_29967" align="alignleft" width="620"] Wanafunzi wa shule hiyo wakimsikiliza Mkurugenzi wa shirika la Kivulini, Yassin Ally kwenye uzinduzi huo.[/caption] [caption id="attachment_29968" align="alignleft" width="620"] Viongozi mbalimbali.[/caption] [caption id="attachment_29969" align="alignleft" width="620"] Maafisa wa ulinzi.[/caption] [caption id="attachment_29970" align="alignleft" width="620"] Wanafuzni wa shule ya wasichana Bwiru wakifurahia jambo kwenye uzinduzi huo.[/caption] [caption id="attachment_29971" align="alignleft" width="620"] Wanafunzi wakimkabidhi zawadi mgeni rasmi.[/caption] [caption id="attachment_29972" align="alignleft" width="620"] Wanafunzi wa shule ya wasichana Bwiru wakikabidhiwa zawadi na mgeni rasmi baada ya kufanya vyema kwenye masomo yao katika shindano la "Best Students of the Year" lililoasisiwa na shirika la Kivulini.[/caption] [caption id="attachment_29972" align="alignleft" width="620"] Wanafunzi wakiwa kwenye picha ya pamoja na mgeni rasmi pamoja na Afisa Elimu Sekondari wilayani Ilemela.[/caption] [caption id="attachment_29973" align="alignleft" width="620"] Wanafunzi wa shule ya wasichana Bwiru wakikabidhiwa zawadi na mgeni rasmi baada ya kufanya vyema kwenye masomo yao katika shindano la "Best Students of the Year" lililoasisiwa na shirika la Kivulini.[/caption] [caption id="attachment_29974" align="alignleft" width="620"] Wanafunzi wa shule ya wasichana Bwiru wakikabidhiwa zawadi na mgeni rasmi baada ya kufanya vyema kwenye masomo yao katika shindano la "Best Students of the Year" lililoasisiwa na shirika la Kivulini.[/caption] [caption id="attachment_29975" align="alignleft" width="620"] Burudani kutoka kwa kikundi cha ngoma asilia, Chapa Kazi kutoka Nyamadoke wilayani Ilemela.[/caption] [caption id="attachment_29976" align="alignleft" width="620"] Shirika la Kutetea Haki za Wasichana na Wanawake KIVULINI.[/caption] [caption id="attachment_29977" align="alignleft" width="620"] Karibu shule ya Wasichana Bwiru iliyopo Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza ili kujifunza kuhusu uanzishwaji wa Viwanda.[/caption]