Friday, October 12, 2012

DIAMOND PLATINUM APIGA KAMPENI YA NGORONGORO CRATER

 



Diamond Platinum ni moja
kati ya wasanii ambao wanafanya vizuri sana katika game la muziki hapa Tzee
hata nje ya Tzee. Habari ambayo tumeipata kuhusu Msanii huyu ni kwamba kwa

siku ya leo ameanza kampeni yake ya Ngorongoro Crater.Baada kupata
taarifa hiyo msanii huyu aliandika ujumbe huu katika site yake baada ya kuanza
kampeni hiyo huyu hapa anafunguka"“Pamoja na kuja kupunguza mawazo
lakini sehemu kama hii inasaidia kuelemisha, mwito wangu kwa watanzania
wenzangu, mashule hata vyuo waweze kuja hapa, inakuwa rahisi zaidi kumfundisha
mtoto kuhusu Simba, Twiga, au bonde la Ngorongoro kwa kumuonyesha hiki kiko
hivi, nadhani kama watoto watakuwa wanasoma kwa vitendo hawawezi kushindwa
mitihani yao kwa sababu kumbukumbu inabaki kichwani kwa kile
walichokiona,”Hayo ndiyo maneno ya mtu mzima

Diamond wa wasafi baada ya kufika Ngorongoro.

No comments: