.

SOMA ALICHOKISEMA KIBANDA KUHUSU WALIOMVAMIA



Akizungumza kwa tabu alipokuwa chumba cha wagonjwa ICU, Hospitalini Moi, alisema, "Nilifika nyumbani kwangu kama saa 6 usiku nikitokea kazini tulikuwa tunafuatilia uchaguzi wa Kenya tukaona hamna la maana.

Nilipofika kwenye lango la kuingia ndani nilipiga honi ili mlinzi anifungulie. Lakini ghafla nilivamiwa na kundi la watu ambao walivunja kioo cha gari langu... Nilitokea kupitia mlango wa abiria lakini sikuweza kukimbia kwani walinikamata na kuanza kunishambulia kwa vitu vizito... niliona kama watu 3 hivi...

Sikufahamu kilichojiri, lakini nilisikia mwingine akimwambia mwenzake afande 'mshuti...mshuti' huyo alipoelekeza mtutu na kujaribu kushuti' ilikuwa kama vile imegoma.

Nikiwa bado niko chini, wakanipiga kwa kitu cha ncha kali kwenye jicho la kushoto, wakaningoa meno na kucha ktk vidole vya mkono wa kulia, walinipiga sana na nilipata maumivu makali. Baada ya kunipiga na kunijeruhi waliniburuza hadi pembeni ya nyumba na kunitupa na wakaondoka, badaye majirani na wasamaria wema walikuja kuniokoa.

HABARI KWA HISANI YA JAMII FORUM

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.