Wednesday, June 19, 2013

KUHUSU ARUSHA LEO POLISI IMESEMA HAYA

TAARIFA YA POLISI KUTOKA ARUSHA

.
.
           Taarifa za sasa kutoka kwenye jeshi la Polisi Arusha kuhusu vurugu za jana June 18 zilizofanya mpaka mabomu ya machozi kupigwa kwenye mitaa mbalimbali ya 87.9 Arusha, ni watu 67 wanashikiliwa kutokana na ishu nzima ya jana ya mkutano wa Chadema.
Polisi wanasema leoleo watu hawa wakiwemo wabunge wanne ambao ni Tundu Lissu, Mustapha Akunai, Mama Nkya na Said Hafizi watafikishwa Mahakamani wakati wowote.

      Polisi wamemtaka Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe popote alipo ajisalimishe ili kulisaidia Jeshi kwa sababu alitamka kwamba ana ushahidi wa kutosha kwamba bomu la juzi lililoua watu kwenye mkutano wa Chadema lilirushwa na Polisi.
Wanasema kama hatopenda kulipa Jeshi la Polisi ushirikiano basi apeleke ushahidi huo kwenye ofisi yoyote ya Serikali anayoiamini au hata kwenye ofisi ya Rais, anaweza kumkabidhi mkuu wa Nchi pia.KUHUSU ARUSHA 

No comments: