Serikali
imeshauriwa kuendelea kuzalisha umeme
kwa njia ambazo ni salama kwa mazingira ikiwa ni pamoja na kuweka kipaumbele
katika matumizi ya umeme wa maji na gesi asilia ambao imetajwa kuwa ndio njia rafiki kwa
mazingira
Wito
huo umetolewa katika semina uliowakutanisha wadau mbalimbali wa nishati nchini
wenye lengo la kuzindua mpango mkakati wa kuzalisha umeme kwa njia ambazo ni
salama kwa nchi kama maji na gesi asilia semina iliyofanyika jijini dar se salaam.
Akizungumza
katika semina hiyo iliyohudhuriwa na wataalam mbalimbali kutoka wizara ya
nishati na madin.wizara ya kilimo,pamoja na wizara sayansi na technologia
mwandaaji wa semina hiyo bw LEORNAD KASSANA
amesema kuwa ili kutunza mazingira lazima serikali iendeleze jiihata zake za
kufua umeme wa maji ambayo ndio njia rafiki kwa mazingira
Bw KASSANA
kuwa serikali ina rasilimali nyingi ambazo kama zitatumika ipasavyo kuzalisha
umeme zinawaza kusaidia katika kuokoa mazingira
Aidha
ameongeza kuwa serikali lazima iwashirikishe wadau katika maswala ya nishati salama
kwani umeme ndio uti wa mgongo wa uchumi wa tanzania.
No comments:
Post a Comment