Akizungumza na wanahabari mchana wa leo, Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ametangaza kuahirishwa kwa uchaguzi wa Udiwani katika kata za Elerai, Themi, Kaloleni na kimandolu Manispaa ya Arusha hadi tarehe 14/7/2013.
Amesema sababu kuu ni hali ya amani bado sio nzuri ya kuruhusu uchaguzi kufanyika kwa sasa.
Itakumbukwa kuwa Uchaguzi wa Kata Hizi ambao ulikuwa ufanyike tarehe 16/6 uliahirishwa hadi tarehe 30/6 kutokana na mlipuko wa bomu kwenye mkutano wa kufunga kampeni wa CHADEMA.
Kampeni hazitakuwepo kwa kipindi hiki hadi tarehe ya Uchaguzi.
NAWASILISHA
No comments:
Post a Comment