.

SOMA REPORT YA DAKTARI WA MUHIMBILI JUU YA JERAHA LA SHEIKH PONDA,WASEMA HAWAJUI ALIPIGWA NA KITU GANI

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU MAJERAHA YA SHEIK PONDA ISA PONDA

dar es salaam 
12/8/2013

sheikh ponda issa ponda (54) alipokelewa hapa ytaasisi ya ya tiba ya mifupa na upasuaji wa mishipa ya fahamu MOI jana tarehe 11/8/2013 saa 7.30 adhuhuri akitokea hospitali ya taifa muhimbili

baada ya kupokelewa alionekana akiwa na majeraha chini ya bega la mkono wa kulia lililokuwa limeshonwa mbele na nyuma

madaktari wetu walifanya uchunguzi na kushauri afanyiwe kipimo cha x-ray ili ubaini kama kuna mvunjiko kwenye sehemu ya jeraha

tathimini ya madactari baada ya kupata majibu ya x/ray ilionyesha alikuwa na mvunjiko bila mifupa kupishana

vivyo hivyo kidonda hakikuwa katika hali nzuri licha ya tiba ya mwanzo na iliamuliwa afanyiwe upasuaji mpya ili kuzuia maambukizi kama kingeachwa hivyo 

KWA HIYO

1-kufwatana na tiba ya awali aliyopata ikiwa ni pamoja na kushonwa jeraha kabla kabla ya kufikishwa moi imekuwa vigumu kujua kama jeraha lilisababishwa na kitu gani

2-kipimo cha x-ray kilionyesha kwamba alikuwa amepata mvunjiko wa mfupa mkubwa wa bega bila mifupa kupishana 

3-hivyo basi sheikh ponda issa ponda anaendelea n matibabu baada ya upasuaji .

                                            mkurugenzi mtendaji

                   taasisi ya mifupa na upasuaji wa mishipa ya fahamu MOI 

                                               - xxxxxxx-

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.