YANGA YAICHAKAZA MTIBWA TAIFA

MSHAMBULIAJI HATARI WA YANGA SAID BAHANUZI AMBAYE ALIKAA KIMYA KWA MUDA MREFU AKIONEKANA KUREJEA KWA KASI SANA KATIKA TIMU YAKE HIYO


           BAADA YA SIMBA JANA KULAZIMISHWA SARE YA GOLI MOJA KWA MOJA JANA NA TIMU YA KOMBAIN YA POLISI JANA KATIKA UWANJA WA TAIFA,WAPINZANIA WAO YANGA LEO WAMEFANYA KILE AMBACHO MASHABIKI WAO WANATAKA KWA KUIADABISHA MTIBWA SUGAR KWA MAGOLI 3 KWA MOJA KATIKA MCHEZO WA KUJIPIMA NGUVU ULIOFANYIKA KATIKA UWANJA WA TAIFA JIJINI DAR ES SALAAM MUDA MFUPI ULIOPITA

            MAGOLI YA YANGA YALIWEKWA NYAVUNI NA MSHAMBULIAJI HATARI SAIDI BAHANUZI KATIKA KIPINDI CHA KWANZA AMBAPO ALIFUNGA GOLI LA KWANZA KATIKA DAKIKA YA 26 BAADA YA KUTOKEA PIGA NIKUPIGE KATIKA LANGO LA MTIBWA
  
         MAGOLI MENGINE YALIFUNGWA NA MCHEZAJI JERI TEGETE KWA PENAT BAADA YA YEYE MWENYEWE KUANGUSHWA KATIKA ENEO LA HATARI ,HUKU BAO LA TATU NALO LIKIFUNGWA NA HUSEN JAVU NA BAO LA KUFUTA MACHOZI LILIFUNGWA NA KISIGA KWA PENANT BAADA YA BEKI WA YANGA KUUNAWA MPIRA KATIKA ENEO LA HATARI

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.