Katibu mkuu wa CCM Mkoa wa Iringa,Ndugu Hassani Mtenga
akizungumza na wanahabari wa Iringa katika ofisi za chama hicho mapema
leo.
KATIBU wa CCM Mkoa wa Iringa
Hassani Mtenga amekanusha chama hicho kuhusishwa na waraka aliodai umesambazwa
na Chadema ukihusu mchanganuo wa matumizi ya Sh Milioni 560 katika uchaguzi
mdogo wa jimbo la Kalenga.
Alisema propaganda za kisiasa
za wapinzani ndio chanzo cha waraka huo kusambaa na kuwaonyesha waandishi wa
habari sahihi kamili ya Naibu Katibu Mkuu wa CCM Mwigulu Nchemba
anayesemekana alisaini waraka huo.
"Kwanza kuna kosa hawa wenzetu
wanafanya, waraka huo una anwani ya Katibu wa CCM Mkoa wa Iringa lakini chini
unaonekana umesainiwa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Mwigulu Nchemba, sahihi
ambayo imegushiwa,” alisema Mtenga
Katika waraka huo wenye kichwa cha
habari kinachosema ‘Malipo ya kamati mbalimbali kwenye ushindi wa jimbo la
Kalenga, umeidhinisha fedha hizo zitolewe kwa viongozi mbalimbali kama
walivyoomba oili zitumike katika kampeni za jimbo.
Waraka huo unaonyesha kuwa CCM
wametumia kiasi cha shilingi milioni 560 kwa ajili ya timu ya ushindi wiki hii
ya mwisho ya kampeni, fedha hizo zimetumwa kutokana na tathimini yenu kuwa ni
hali mbaya kwetu kwa barua yenu yenye kumb Namba CCM/IR/VOL11/096.
“Hakikisha kiwango hiki
kinwafikia walengwa wote wafuatao kwa uwiao tuliokubaliana kulingana na
maeneo yao na wao wazigawe kwa mabalozi wetu kwenye kila kitongoji na kata
apewe Balozi Sh850,000, Mama Galinoma Sh Milioni 80, Mama Ray (Ulanda) Sh
Milioni 60, wenyeviti wa kata wa CCM kila mmoja Sh Milioni 20, makatibu wa kata
kila mmoja Sh Milioni 8, makatibu wenezi CCM kila mmoja Sh Milioni 14 na Kamati
ya ushindi Nzihi Sh Milioni 108,” sehemu ya waraka huo inasema.
Mtenga alisema lengo la kusambazwa
kwa waraka huo lilikuwa kuwaaminisha wapiga kura wa Kalenga kwamba kuna fedha
zimetolewa na CCM kwa ajili yao lakini zimeliwa na watu wanaotajwa katika
waraka huo.
Alisema kuna kila dalili kwamba
waraka huo uliandaliwa na Chadema kwa lengo la kuwarubuni wananchi wa jimbo la
Kalenga wakose imani na CCM.
Wakati huo huo CCM kimempa
siku 7 Kamanda wa Polisi wa Wilaya ya Iringa, OCD Sifael Pyuza kuwataka
radhi kwa madai ya kuwadhalilisha katika ofisi za chama hicho mkoani hapa baada
ya kuwafanyia uchunguzi bila kuwa na kibali maalum.
Kamanda Pyuza anatuhumiwa na chama
hicho kukihusisha na mchezo mchafu wa siasa kwa kuficha watu ndani ya jengo la
ofisi yake waliokuja katika uchaguzi mdogo wa Kalenga uliofanyika machi 16 na
ccm kuibuka kidedea.
Katibu wa CCM Mkoa wa Iringa,
Hassan Mtenga aliyasema hayo jana wakati akizungumza na waandishi wa
habari ofisini kwake kuwa , Machi 16 mwaka huu kamanda huyo alituma
makechero wa jeshi hilo katika ofisi za CCM za mkoa wa Iringa waliotumia mabavu
kupekua ofisi moja baada ya nyingine bila kuwa na kibali halali.
Alimtaka kamanda huyo kuwaomba
radhi baada ya tuhuma yake dhidi yao kubainika haina ukweli.
na chama cha mapinduzi hakiwezi
kukaa kimya kwa udhalilishaji huu uliofanywa na mkuu wa upelelezi wa
wilaya kwa sababu jambo hilo ni sawa na kukiingiza chama cha
mapinduzi katika kashfa ya mchezo mchafu wa kisiasa.
upande wake Kamanda wa Polisi
wa Mkoa wa Iringa, Ramadhani Mungi alisema hana taarifa yoyote kuhusiana na
madai ya chama hicho lakini yupo tayari kuyapokea na kuyafan |
No comments:
Post a Comment