Kituo cha haki za binadamu mapema hii leo imezindua ripoti yake walioipa jina la ripoti ya haki za binadam na biashara huku ripoti hiyo ikifichua mambo makubwa katika maeneo makuu sita yaliyofanyiwa utafiti katika mikoa kumi na tano ya Tanzania bara
Reporti hiyo iliyojikita katika maeneo makuu sita ambayo ni haki za ajira, Haki za Ardhi,, Kodi, uwajibikaji wa makampuni kwa jamii na serikali,, Haki za mazingira na Haki za Kijinsia amebaini kuwa katika kada ya kodi Taifa kwa kila mwaka Linapozeta jumla ya USD trion moja kutokana na mifumo mibovu ya fedha,
Ripoti hiyo imefafanua kuwa hasara hiyo ya matrioni ya mapesa yanatokana na makampuni mbalimbali kukwepa kulipa kodi pamoja na misamaha ya kodi ambayo haina tija kwa taifa ,
Mfano, kwa kila mwaka kati ya 2010 na 2012 msamaha ya kodi ilifikia kiasi cha bilioni 600 au 14.1 asilimia ya makadilio ya makusanyo hii ni hatari kwa taifa kukosa mamilioni yote hayo kwa kipindi cha mwaka huo, aliongeza Mkurugenzi wa Kituo cha haki za binadam hapa nchini DK Hellen Kijjo Bisimba wakati akiwakilisha taarifa ya ya ripoti hiyo kwa ufupi mbele ya wadau waliokutana jiji Daresalaam mapema hii leo
Naye kwa upande wake Mkurugenzi wa Mazingira ofisi ya makamu wa Rais,Dk Jurius Ningu akizindua Taarifa hiyo, amesema Taifa sasa kuna haja ya kujiangalia upya namna ya kusamehe kodi kwa makampuni makubwa yanayoingiza bidhaa zao hapa nchinikuwa anaeumia kwa kiasi kikubwa ni mwananchi mlala hoi anayeilipa kodi yake kwa mfumo wa Vat,
Amesema fedha inayopotea kwa mwaka ni fedha kubwa ambayo haipaswi kuifumbia macho hata kidogo, ukizingatia kuwa taifa bado ni maskini, linalohitaji kujijenga kwa kiasi kikubwa kupia kodi.
Mgeni rasmi katika uzinduzi wa ripoti za haki ya binadam na biashara Dkt Julius Ningu Toka ofisi ya makamu wa rais akifafanua jambo mbele ya wadau wa haki za binadam mapema hii leo, |
Katika kada ya Haki za ajira hapa
nchini, utafiti huo unaonyesha kuwa, kunachangamoto kubwa ya kufuata
viwango vya ndani na kimataifa, huku waajiri wengi wakionekana kukwepa
kuajiri wafanyakazi wao, na wengine kuwabadili majina ya wafanyakazi wao
kwa kila baada ya miezi miwili ili kukwepa kulipa NSSF za waajiriwa
wao,
Kama kwenye sekta ya ajira utafiti unaonyesha kuwa zaaidi ya 80% ya wafanyakazi hpa nchini hawana mikataba ya kufanya kazi na chini ya 30% walionekana kuwa na mikataba lakini mikataba hiyo bado imeonyesha udhaifu mkubwa na manyanyaso makubwa kwa waajiriwa hao, Alisema DK Kijjo Bisimba
Kama kwenye sekta ya ajira utafiti unaonyesha kuwa zaaidi ya 80% ya wafanyakazi hpa nchini hawana mikataba ya kufanya kazi na chini ya 30% walionekana kuwa na mikataba lakini mikataba hiyo bado imeonyesha udhaifu mkubwa na manyanyaso makubwa kwa waajiriwa hao, Alisema DK Kijjo Bisimba
Mgeni rasmi Akizindua Taarifa hiyo, kila mdau alifanikiwa kupata taarifa hiyo hapohapo |
Wadau pamoja na viongozi wa kituo cha haki na binadam wakipata picha ya pamoja mapema hii leo,HABARI KWA MSAADA WA FULLHABARI BLOG. |
No comments:
Post a Comment