Thursday, April 17, 2014

ASASI ZA KIRAIA ZAUNGANA NA UKAWA,WAKUTANA NA WANAHABARI WATOA TAMKO KALI KWA RAISI,LISOME HAPA

Mwenyekiti wa asasi zisizo za kiserikali Bw.Irinei Kiria, akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari juu ya Tathimini  zilizofanywa na asasi za kiraia kuhusu mwenendo wa mchakato wa katiba mpya unaoendelea katika bunge la katiba mjini Dodoma,Katika tahimini yao hiyo, umoja huo umegundua madhaifu mengi sana ambayo kama hayatapatia ufumbuzi wake basi katiba mpya yenye kumjali mtanzania ni Ndoto kupatikana. 
        
 Na Karoli Vinsent

       SIKU moja kupita baada ya Umoja wa Katiba ya Wananchi UKAWA,kususia vikao vya bunge maalum la Katiba  kutokana na uonevu kutoka kwa wajumbe wa Chama cha Mapinduzi CCM.

   Hivi, leo  nao umoja wa Asasi za Kiraia AZAKI  umeibuka na kumtaka Rais Jakaya Kikwete kuvunja  Bunge la katiba maramoja,kutokana na wajumbe hao kuanza kujadili katiba yenye maslai yao na kusahau wananchi ambao ndio waliowatuma.


Hayo,yalisemwa leo Jijini Dar es Salaam na Mweyekiti wa umoja wa umoja wa asasi za Kiraia AZAKI, Irenei  Kiria wakati wa mkutano na Waandishi,ambapo alisema hawajafurahishwa na mijadala ndani  ya Bunge la Katiba,

“Sisi umoja wa Asasi za Kiraia hatujaridhishwa na mijadala ndani ya Bunge Maalum la kutunga Katiba,mijadala ambayo imepoteza Utaifa na badala yeke kujikita kwenye kutoheshimiana,ubabe,ubaguzi,vijembe na Vitisho kutoka kwa wajumbe”

“Tunaona kwamba Mwendendo wa Mijadala ni kuelekea kuteta maslahi ya watawala na vyama vya siasa badala ya maslai ya utaifa na ustawi wa wananchi”Alisema Kiria

Kiria,alizidi kusema wao hawajalizishwa na maauzi ya wajumbe hao wa bunge hilo kupendekeza kufuta vitu muhimu kwenye Katiba.
“kwamba kitendo cha Baadhi ya Wajumbe kupendekeza kutoa maneno,uwajibikaji,uadilifu,uwazi katika kipengele cha tunu za Taifa inatia shaka kama nia ya Bunge Maalumu la katiba na kutuletea katiba itakayotatulia matatizo yao”

“Vilevile pia hatujafurahishwa na kufungiwa Tovuti ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba.Na hakuna juhudu zaSerikali kuwafikishia wananchi Rasimu ya pili ya Katiba,kwahiyo sisi tunaona kwa Rais Jakaya Kiwete avunje Bunge hili la Katiba”aliongeza Kiria.

Kwa Upande wake Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za binadamu Bi Kijo Bisimba naye alisema Rais Jakaya kiwete amepwaya katika kusimamia mchakato huo wa Katiba kutokana na Kitendo chake cha kufuata matakwa ya Chama chake.
“Kiukweli Rais Kikwete wakati ananza mchakato huu hadi kuunda Tume ya kukusanya maoni  alianza vizuri,Lakini amekuja kuchemsha baada ya kutoa hutuba yake wakati akifungua bunge Maalum la katiba ameonekana wazi kabisa anaanza kufuata matakwa ya chama chake,na yeye ndio alianza kuharibu mchakato wote wa katiba”alisema Bisimba.
Naye,Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba Deus Kibamba,ambaye taasisi yake ndio inayounda AZAKI,alisema Rais Kiwete avunje bunge hilo la Katiba kutokana na Mambo yanayoendelea katika bunge hilo.

“Kiukweli wote mashahidi akuna kinachofanyika mule Bungeni zaidi ya vijembe tu  na kila mtu akitetea maslai ya chama chakee na kuwasahau wananchi,na Hata Kauli aliyoitoa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu wa Bunge), William Lukuvi ni wazi hakuna kinachojadilwa bungeni,na kama rais Kikwete anamapenzi mema na nchi yake na kujenga heshima basi avunje bunge hilo la katiba haraka sana”alisema Kibamba

Haatua hii ya AZAKI imekuja siku moja tu kupita baada ya umoja wa Katiba ya Wananchi UKAWA kususia bunge hilo la katiba kwa kile wananchodai ni ufedheheshaji na kuwagawa wananchi kutoka kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu wa Bunge) kutokana na Kauli zake.
Hatua ya kususia vikao hivyo ilitolewa na Profesa Lipumba jana bungeni ambapo alianza kwa kunukuu Gazeti la Mwananchi la Aprili 14, mwaka huu katika sehemu inayosema;
 “Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Uratibu na Bunge) ameanza kampeni kanisani kwa kuwataka wananchi kupinga serikali tatu zilizopendekezwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba, vinginevyo nchi itatawaliwa na jeshi kwa kuwa serikali ya muungano itashindwa kuwalipa mishahara wanajeshi.”
Alisema yeye ni muumini wa dini ya Mwenyezi Mungu lakini anaafiki mapendekezo yaliyoletwa bungeni hapo na Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyoundwa na Rais.
“Hii ni kauli ya Waziri Lukuvi ndani ya Kanisa la Methodist wakati wa sherehe ya kumsimika Mchungaji Joseph Bundala kuwa Askofu na Waziri Lukuvi alikuwa anamwakilisha Waziri Mkuu.”
Alisema inasikitisha kwa sababu kauli hiyo inafanana na ya Rais Jakaya Kikwete aliyoitoa wakati akihutubia Bunge Maalumu.
Alisema kauli za Lukuvi zinatisha baada ya kusema Wazanzibari ambao wanataka kuwa na nchi yao hawawezi kujitegemea, bali wanataka wapate nafasi ya kujitangazia kuwa ni nchi ya Kiislamu.
“Waziri anaweza kusema hivyo ndani ya kanisa? Kawahamasisha mpaka yule kiongozi wa kanisa akasema ili kudumisha Muungano bora Katiba ya Zanzibar ifutwe ili iwepo moja ya nchi moja ambayo inadumisha Muungano,” alisema.
“Kama ndugu zetu wa Zanzibar wangekuwa wanahitaji serikali moja tungekuwa na utaratibu mzuri tu, lakini siyo wanachama wa CUF, siyo wa CCM, Wazanzibari wote hawataki muungano wa serikali moja,” alisema.
Alisema Tume ya Mabadiliko ya Katiba imetoa mapendekezo ya serikali tatu kutokana na ukweli huo. “Hoja zilizoletwa hapa ni hoja za serikali moja, si hoja za serikali mbili lakini wenzetu moja hawataki, kwa hiyo tunahitaji Muungano ambao tutakuwa na maridhiano ya pande zote mbili,”

No comments: