Thursday, April 17, 2014

TIGO YAONYESHA UPENDO KWA WAHANGA WA MAFURIKO,YATOA ZAIDI YA MILION 20 KUWASAIDIA

Mwakilishi wa kampuni ya tigo katika makabidhiano hayo bi WAINDE SHISAEL akimkabidhi kaimu naibu katibu mkuu wa shirika la msalaba mwekundu bi BERTHA MLAY msaada wa vyakula vyenye thamani ya shilingi milion nne kwa ajili ya kuwasaidia wahanga wa mafuriko katika maeneo mbalimbali ya mvua nchini tanzania kwa kipindi hiki ambapo mafurikoyamekuwa yakitokea mara kwa mara

Wafanyakazi mbalimbali wa kampuni ya tigo tanzania wakiwa katika makabidhiano hayo katika ofisi za shirika la msalaba mwekundu nchini tanzania
vyakula vyenye thamani ya shilingi milion 4

kaimu naibu katibu wa redcross tanzania BERTHA MLAY  akizungumza na wanahabari jijini dar es salaam kuhusu msaada huo walioupata kutoka katika kampuni ya mawasiliano nchini tanzania TIGO  ambapo amewasifu sana kwa kuwa na moyo wa kutoa kwa watu wanaohitaji msaada ambapo amesema kuwa msaada huo utawasaidia sana katika kuwasaidia watu hao huku akitoa wito kwa makapuni mengine kuiga mfano huo wa tigo
Wafanyakazi mbalimbali wa shirika la msalaba mwekundu na tigo wakiwa katika makabidhiano hayo yaliyofanyika jijini dar es salaam mapema leo

Kampuni ya mawasiliano ya tigo tanzania leo imetoa msaada wa fedha na vyakula kwa shirika la msalaba mwekundu tanzania kwa ajili ya watu waliokumbwa na mafuriko jijini dar es salaam na mikoa mingine ambayo imekumbwa na ,mafuriko hayo,vitu vilivyotolewa ni pamoja na pesa taslim million 20 nna laki saba,pamoja na vyakula vyenye thamani ya shilingi million nne.msaada huo umetolewa baada ya kutokea kwa mafuriko maeneo mbalimbali jijini dar es salaam na mikoa mingine hapa nchini

No comments: