Monday, April 28, 2014

BREAKING NEWZZ---UVAMIZI WA BANK YA BARCLAYS KINONDONI NI UZUSHI MTUPU,KAMISHNA KOVA ASEMA WALIJIIBIA WENYEWE,13 WATIWA MBARONI WAMO WAFANYAKAZI WA BANK HIYO--SOMA KISA KIZIMA HAPA

Kamishna wa polisi kanda maalum ya dar es salaam SULEMAN KOVA akizungumza na wanahabari jijini dar es salaam

        Jeshi la Polisi Kanda Maalum D’Salaam linawashikilia watuhumiwa 13 ambao wanahusishwa na tukio la ujambazi lililotokea tarehe 15/4/2014 majira ya saa tatu na nusu asubuhi katika Tawi la Benki hiyo Kinondoni.
       
        Watu wenye silaha aina ya SMG na Bastola waliingia ndani ya benki ya Baclays na kupora kiasi cha pesa T.Shs.390,220,000, USD 55000, UERO 2150 na Pound 50.  
     
     Majambazi waliwatishia kwa silaha watumishi wa benki hiyo na kuwaweka chini ya ulinzi na hatimaye kutoroka na pesa hizo kwa kutumia pikipiki aina ya Fekon. 
    
      Awali majambazi hayo yalifika katika benki hiyo wakiwa na magari 2, gari moja aina ya OPA lenye namba T.421 BQV rangi ya Silver ambayo sasa imekamatwa. 


Wanahabari mbalimbali wakiwa kazini katika mkutano huo wa kamishna kova na wanahabari leo jijini dar es salaam


          Majambazi hao walianza kusakwa na vikosi mbali mbali vya Jeshi la Polisi ikiwa ni pamoja na Kikosi Maalum (Task Force) ambacho ni Maalum kwa kuzuia na kupambana na wizi katika mabenki jijini D’Salaam.  Kati ya watu waliokamatwa ni pamoja na Meneja wa benki katika Tawi hilo
       
        1. ALUNE D/O KASILILIKA @ MOLLEL, MIAKA 28, MKAZI WA KIMARA BONYOKWA, ambaye uchunguzi wa kina unaonyesha kwamba Meneja huyu alishirikiana na mfanyakazi mwenzake ambaye ni Meneja Operesheni wa benki hiyo aitwaye 2. NEEMA D/O BANDARI @ BACHU kwa kula njama na watu wengine na majambazi ambao kwa pamoja walifanikisha tukio hilo la wizi wa fedha katika tawi hilo.  Aidha katika tukio hilo imegundulika kwamba robo tatu ya fedha zote zilizoibiwa zilichukuliwa kabla ya siku ya tukio la ujambazi tarehe 15/4/2014.  
  
     
     Siku hiyo ya tarehe 15/4/2014 ilikuwa ni utekelezaji ili kukamilisha njama hizo.  Watuhumiwa wengine waliokamatwa katika tukio hilo ambao ni majambazi ni:
3.      FREDRICK S/O LAZARO miaka 19, mkazi wa Manzese
4.      KAKAMIYE S/O JULIUS miaka 31, mkazi wa Kinondoni
5.      IDDI S/O NGUVU @ HAMISI miaka 32, mkazi wa Kinondoni
6.      SEZARY S/O OSWARD MASAWE @ MSOLOPA
7.      BONIFACE S/O NDARO @ MUUMBA miaka 29 mkazi wa Kijitonyama
8.      ERASMUS S/O BERNARD MROTO @ MENYEE miaka 38 mkazi wa Magomeni
9.      DEO S/O ISDORI OLOMY miaka 32, mkazi wa Manzese Darajani
10.    MOHAMED S/O ATHUMANI @ SALUM miaka 31, mkazi wa Kimara Stopover
11.    JOSEPH S/O MKOI miaka 33, mkazi wa Kimara Stopover
12.    LUCY D/O AMOS @ MACHA miaka 30,  mkazi wa Tabata
13.    GRACE D/O AMON @ MACHA miaka 39, mkazi wa Kibaha
Aidha baadhi ya watuhumiwa waliokamatwa wamehojiwa na kukiri kuhusika na wizi huo na walipopekuliwa walipatikana na fedha kiasi kidogo ambazo ni sehemu ya mgao waliopata baada ya tukio hilo. Vile vile kabla ya tukio imebainika kuwa kulikuwa na vikao mbali mbali vya maandalizi ya kufanikisha tukio hili kabla ya tarehe 15/4/2014 ambayo ni siku ya tukio.

Upelelezi wa shauri hili bado unaendelea, tunaomba wananchi/raia wema waendelee kusaidiana na Jeshi la Polisi kwa kutupatia taarifa ili tuweze kuwakamata wote waliohusika na tukio hilo ili sheria iweze kuchukua mkondo wake.

No comments: