Thursday, April 24, 2014

KOCHA MPYA STARS KUTUA JUMAMOSI



Kocha Mkuu mpya wa Taifa Stars, Martinus Ignatius Maria maarufu kama Mart Nooij anatarajiwa kuwasili nchini Jumamosi alfajiri (Aprili 26 mwaka huu) tayari kwa ajili ya kuanza kazi ya kuinoa timu hiyo.

Nooij (59) atawasili saa 7.20 usiku kwa ndege ya Ethiopia Airlines ambapo anatarajia kukutana na waandishi wa habari Jumamosi mchana, saa chache kabla ya kuanza mechi ya kirafiki kati ya Taifa Stars na Burundi itakayochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam


No comments: