Thursday, April 24, 2014

HABARI ILIYOKUWA GUMZO NCHI NZIMA---BAADA YA TUHUMA ZA WAZIRI LUKUVI KWA UAMSHO,UAMSHO WAJITOKEZA MBELE YA WANAHABARI LEO WATOA ONYO KALI,WATAKA KUMPANDISHA KIZIMBANI,SOMA TAMKO LAO HAPA



Na Karoli Vinsent
     
     KAULI ya wahenga inayosema “Mdomo ulimponza kichwa”sasa ndiyo yanamkuta sasa, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi,

          Baada ya leo Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislam kuibuka na kumtaka Rais Jakaya Kikwete kumfukuza Kazi Waziri Lukuvu,na kama Akikaida basi,Umoja huo hautamburuza Mahakamani.

        Kauli,hiyo kali imetolewa Jijini Dar es Salaam,na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislam ,Abdallah Said Alli,wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari,ambapo alisema wamesikitishwa sana na Kauli za Kichochezi na kuligawa Kidini Taifa,na kupakizia sifa mbaya umoja huo.


       “Sisi tumesikitishwa sana na Kauli aliyoitoa Waziri mkubwa kama Yule,aliyoitoa Kanisani na Baadae akaja kuitoa Kwenye Vikao vya Bunge la Katiba,eti akitushutumu sisi kwamba ndio tunahusika na vitendo  Viovu,na vilevile kutuhusisha na Chama cha Wananchi CUF”

       “Mpaka Hivi sasa Hakuna Ushahidi wowote  uliowahi,kutolewa na Kuthibitishwa na kuihusisha UAMSHO na Vurugu zozote zilizowahi, kutokea pale Zanzibar”alisema Alli

        Vilevile,Katibu huyo alisema kwa sasa wameamua Kumwandikia Mwenyekiti wa Bunge Maalum La Katiba Samweli Sitta.

     “Tumemwandikia Barua Mwenyekiti wa Bunge la Katiba Samweli Sitta ili atuambie ukweli kauli aliyoitoa Waziri Lukuvi,inahulali au la na tumemwambia ukweli sisi hatuhusiki na upande wowote wa Chama cha Kisiasa”

       “Kwasabu Jumuiya Hii imesajiliwa kihali kabisa na Serikili ya Mapinduzi ya Zanzibar kufanya shuguli za kutoa elimu ya Dini ya Kiislam, sasa inakuwaje waziri mkubwa,kama huyu anaongea Habari za Kichoche Serikali inamwangalia”

        Aidha Katibu huyo alisema kwa sasa Wanamuomba Rais Jakaya Kikwete amfukuze kazi au amwajibishe Waziri Lukuvi.na kama Rais akipuuzia Basi umoja huo utamfikisha Mahakamani ili akathibitishe kile alichoongea pale Bungeni.

         Kwa Upande wake Naibu Katibu Elimu na Habari  wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislam ,Saidi Amour Salim,alisema Waziri Lukuvi ni mtu wa kupigwa vita na asiyetakiwa popote kwa Vitendo vyake vya kuligawa Taifa na kupeleka nchi kwenye machafuko.

     “Serikili naishangaa kwanini wanamfumbia macho waziri huyo wakati anatugawa taifa.tena ndugu zangu anasema UAMSHO ni taasisi ya Kisiasa,wakati sio kweli tena nataka kumwakikishia Lukuvi,Baada ya Rais Kikwete kufanya Mabadailiko Jeshi la Polisi Zanzibar na kumteua Kamanda, nay eye ametuita kwa Amani na kutuomba tukatafute njia ya kufanya Kazi kwa Amani”alisema Salim

        Kauli hiyo inayodaiwa na Jumuiya hiyo ilitolewa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi,Bungeni jijini Dodoma wakati alipotakiwa kutoa ufafuzi juu ya kauli zake alizozitoa kanisani.

         Ambapo,lukuvi Mambo mengi wanayoyasema wanachama wa CUF ndiyo yanayosemwa na taasisi hiyo, hivyo kwa hofu yangu binafsi, sina shaka Uamsho ni CUF kwani hata Wazanzibar wenyewe wanajua hilo,’’ alisema.

      ‘’ Hatujawahi kuona Chama kinachojitayarisha kuchukua madaraka kinatumia mgongo wa dini kufanya siasa. Hii si sahihi, kwanini nisiwe na hofu na kusema,’’ alisisitiza

        Akizungumzia Jeshi kuchukua madaraka, Lukuvi alisema hofu yake hiyo imetokana na rasimu ya katiba, ambayo inapendekeza kuwepo kwa serikali tatu, jambo ambalo serikali moja ya Muungano vyanzo vyake vya mapato havikuwekwa wazi.

         “Haya yalikuwa ni mawazo yangu binafsi na sikuwa na shida kuyaeleza na nitaendelea kuyaeleza na kisiwe chanzo cha wanachama wa UKAWA kudai kuwa hiyo ni lugha ya uchochezi.

       “Hivi kati ya mimi na Maalim Seif (Katibu Mkuu wa CUF) nani ni mchochezi ? Mbona hawakugomea kauli yake aliyoitoa Kibanda Maiti kuwa Rais Kikwete atamtuma Mkuu wa Majeshi Mwamunyange kwenda kupindua nchi iwapo serikali tatu zitapita,’’ alisema lukuvi.



No comments: