Thursday, April 24, 2014

KUZIMWA KWA MAANDAMANO YA UKAWA,SIRI NZITO NDANI YAKE,SOMA HAPA



Na Karoli Vinsent
       
      SIRI ya Serikali kuzima maandamano pamoja Mikutano ya Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA)Nchi nzima,HABARI24 imedokezwa siri hiyo.
         
        Sababu hiyo ni ya kuwakataza UKAWA kufanya mikutano nchi nzima mpaka sherehe za Muungano zitakazomalizika,ambapo sherehe hizo zinatarajiwa kufanyika mwishoni mwa wiki hii
       
        Chanzo hicho kilisema Sababu ya Serikali pamoja na Chama cha Mapinduzi CCM,kufanya hivyo inalengo ya kumpa nafasi Rais wa Tanzania Bara Jakaya Kikwete,ambaye  anatarajiwa kutoa hutuba katika Sherehe hizo, na vilevile itawafanya UKAWA  kukosa nguvu kwa Wananchi.

       
         “Ujue serikali inaakiri sana ndio maana tumekataza mikutano yote ya hawa Jamaa UKAWA nchi nzima ili mpaka Rais atakapo toa hutuba kali sana, ambayo itawafanya umoja huo ukose Hoja ya kuwadanganya wananchi,kwani Serikali ikiwaachia Hawa wajamaa waanze kupita nchi nzima Harafu Rais Kikwete aje kutoa hutuba,itakuwa haina maana”kilisema Chanzo hicho
        
         Umoja ,huo wa Katiba ya Wananchi ambao ulitakiwa kufanya Mikutano pamoja na Maandamano Nchi nzima yenye Lengo ya kuwaelimisha Wananchii Juu ya kile wananchokiita ni kukataliwa  Rasimu ya pili Buge Maalum la Katiba.
        
          Vilevile Sababu nyingine ya Umoja  kuwaeleza Wananchi juu  Kauli ambayo ya Kichochezi na kuligawa Taifa kidini aliyoitoa,  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi alipokuwa kanisani mjini Dodoma .
         
           Chanzo hicho kizidi kusema Rais Kikwete ameshtushwa sana na Kufadhaika kutokana na hatua waliofanya UKAWA ambayo  ilimpa wakati mgumu sana kushindwa cha kufanya.

      “Kwa hatua hii waliofanya hawa watu,Rais amekosa njia ya kufanya Badala yake ameamua kuwaambia Ukweli wananchi katika, siku hiyo ya Sherehe za Muungano ili Umma uamue wenyewe juu hali iliyopo”

        “Ukiangalia mwenyewe sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya 2011 pamoja na marekebisho yake ya 2012 na 2013 inawataja Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kuwa Wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba kwa mujibu wa nafasi zao”.

       “Kadhalika sheria hiyo inampa Rais mamlaka ya kufanya uteuzi wa wajumbe 201 kutoka makundi mbalimbali, lakini haitaji sifa wanazopaswa kuwa nazo wajumbe hao.

       Hata kama sheria ingekuwa inaruhusu kufukuzwa au kusitishwa kwa ujumbe wa wabunge hao, hakuna sababu ya msingi ya kuwachukulia hatua hiyo. Na unafikili hata wewe ungekuwa Rais Kikwete Ungefanyaje maana Sheria haikuruhusu hata kuwaengua UKAWA bungeni na kuteua watu wengine”Kilisema Chanzo hicho Ukawa, walikawataliwa kufanya mikutano yao na Jeshi la polisi nchini ili kupisha Sherehe za muungano.

       Umoja huo wa Ukawa  unatokana muunganiko wa vyama vya CUF, Chadema, NCCR Mageuzi, NRA, NLD na baadhi kutoka kundi la 201.am

bapo kwa kauli moja walisema Hawatarudi tena kwenye vikao hivyo vya Bunge

No comments: