Thursday, April 24, 2014

TIGO YAINGIA MAKUBALIANO NA FACEBOOK,SASA UNAWEZA KUTUMIA FACEBOOK BUREEE KWA LUGHA YA KISWAHILI KATIKA SIMU YAKO MUDA WOWOTE.

Mkurugenzi wa FACEBOOK wa ushirikiano na ukuaji wa kimataifa NICOLA DE ELIA pamoja na mkurugenzi mkuu wa tigo DIEGO GUTIEREZ wakizungumza katika hafla hiyo ya kuzindua huduma hiyo rasmi leo jiji dar es salaam


         Kampuni ya mawasiliano ya simu za mkononi ya tigo leo imetangaza rasmi kuingia katika Ushirikiano mkubwa na kampuni maaarufu ya FACEBOOK ambapo wateja wake wote wataweza kupata huduma za facebook kwa lugha ya kiingereza na kwa mara ya kwanza kwa lugha ya Kiswahili kupitia simu zao za mkononi.

          Kwa mujibu wa mkurugenzi wa mtandao wa Tigo DIEGO GUTIEREZ amesema kuwa  hii ni kwa mara ya kwanza kwa mtandao wa facebook kupatikana bila malipo katika eneo hili la Africa mashariki.

      Akizungumza katika uzinduzi wa huduma hiyo mkurugenzi huyo wa tigo amesema kuwa hii inamaanisha kwamba wateja wa tigo kwa mara ya kwanza watakuwa na uwezo wa kutumia facebook kupitia simu zao za mikononi bila kukatwa gharama za aina yoyote hivyo kuwawezesha kuungana na wateja zaidi ya million mbili wa wanaotumia mtandao huo hapa nchini Tanzania.

             Amesema kuwa hii pia ni kwa mara ya kwanza kwa mtandao wa kijamii kama facebook kupatikana kwa lugha ya kuswahili lugha ambayo inayotumika na watanzania wote ambapo amesema kuwa ni njia nzuri ya kuitangaza lugha hiyo kimataifa zaidi.
           Naye mkurugenzi wa FACEBOOK wa ushirikiano na ukuaji wa kimataifa NICOLA DE ELIA amesema kuwa wanayo furaha kubwa sana kwa kushirikiana na tigo kwa mara nyingine tena na kuwapatia watanzania wengi zaidi uwezo wa kuwasiliana kupitia utumiaji wa bure wa data katika app ya facebook na tovuti ya simu na sasa katika lugha ya kuswahili.


     Mkakati huu ni muendelezo  wa mpango wa facebook unaoitwa internet.org uliozinduliwa na muasisi wa mtandao huo MARK ZUCKERBERG

No comments: