Saturday, April 12, 2014

RAISI WETU JAKAYA MRISHO KIKWETE,TUNAOMBA USOME HAPA.



Na Karoli Vinsent

              VITENDO vya kutapanya  madaraka na kurundika vyeo kwa Makada wa chama cha Mapinduzi CCM,kunavyofanywa na Rais jakaya Kikwete,kunazidi kuibua kelele kutoka kwa wananchi huku wengi wao wakiishia kuumia kutokana na mambo yanayoendele hapa nchini.
         
           Uchunguzi uliofanywa na Mwandishi wa Mtandao huu umebaini Mikoa ya Rukwa na Iringa.na Wilaya za kiteto,hazitakuwa na Viongozi wa Serikali(Wakuu wa Mkoa na Wilaya) kwa kuwa takribani miezi saba watakuwa wakishiriki vikao vya  Bunge maalum la katiba,ambalo wiki chache litafuatiwa na Bunge la bajetila serikali ya Jamhuri wa muungano wa Tanzania.


          Ni dhahiri kumalizika kwa bunge hilo,itakuwa mwanzo wa kuanza kwa mkutano mrefu wa bunge la bajeti ambalo litachukua miezi miwili.
       Kwa mujibu wa Chanzo cha chetu kinasema kwa muda wote huo,mikoa ya Iringa na Rukwa haitakuwa na viongozi wake na wakuu katika mikoa na Wilaya,
       
          Wilaya za Uyui,Meatu na kiteto,hazitakuwa na Wakuu wake kwa kuwa viongozi wake watakuwa wakiishi mjini Dodoma katika vikao vya Bunge la bajeti na la Katiba.
          
         Sababu ya kutokuwepo katika nafasi zao za utawala ni kutokana viongozi hao kuwa katika nafasi ya Viti maalum ungeni,viongozi hao ni Stella Manyanya ambae ni Mkuu wa mko wa Rukwa,Christina Ishengoma vilevile naye ni mkuu wa mkoa wa Iringa.

            Kwa upande wa Wakuu wa Wilaya Ya Kiteto Rose Kamili, Mkuu wa  Wilaya  ya Meatu na Lucy Mayenga mkuu wa Wilaya Uyui.

            Kuwepo kwa Viongozi hawa mjini Dodoma,kumetoa Mwanya kwa Wafanyakazi kutoka katika Halmashauri hizo kuanza kufanya vitendo vya kifisadi huku wananchi wakiteseka kutokana na kutokuwepo kwa Usimamizi kutoka kwa viongozi hao.

             Akizungumza,na mwandishi wa mtandao huu,mmoja wa wafanyakazi kutoka katika Wilaya  ya Meatu,ambaye  amekataa kutaja Jina lake kwenye Mtandao huu,amesema kwa sasa Huduma za kwa sasa haziendi vizuri kutokana na Watumishi kuzembea kutokana na mkuu huyo kutokuwepo ofisini.

       “Ndugu Mwandishi katika familiya yoyote hasipokuwepo Baba  basi akuna kinachofanyika,ndio maana hata hapa leo huduma zinakwenda taratibu,na watu wamegeuza Halmashauri hii kuwa uwanja wa Soga tu”

      “Huku watu wakija kupata huduma hususani waalimu kusota tu,na kama viongozi hawa wangekuwepo basi huduma zisingekuwa legelege hivi”alisema Mtoa Taarifa hiyo

         Duru za kisiasa zinasema wa kulaumiwa kwa hali hiyo ni Rais Jakaya Kikwete ambaye amekuwa akitapanya madaraka kwa watu huku akijua mtu anaempa uongozi Teyali ni kiongozi sehemu nyingine.

         Rais Kikwete amekuwawa akiwatajirisha watu wachache kwa kitendo chake hicho, huku wananchi wakiwa wanaumia na hali hiyo kutokana na ufanisi wa kazi kuwa mdogo kutokana na viongozi hao kushindwa kufanya kazi mbili kwa wakati mmoja.

          Huku  Taifa hili likiwa na Wasomi wengi ambao wamekuwa wakiangaika kutokana na Tatizo la ajira,huku yeye akijinadi kuwa ni mtatuzi wa tatizo hilo.lakini la ajabu tumeshuudika katika utawala wake amekuwa akiwapa makada wa Chama chake kazi mbili kwa wakati mmoja,huku akisau ahadi zake.

            Nikiwa na Tafakari kuhusu kuandika makala hii kutokana na Unyama huu kwa Watanzania kwa kutapanya Madaraka kunavyofanywa na Rais Kikwete.
           
          Hivi,leo tumeshuudia,Rais huyu huyu Kikwete amemteua Waziri wa Nchi Ofisi Rais,kazi maalum.Profesa Mark Mwandosya kuwa mkuu mpya wa Chuo Kikuu cha Sayansi cha Sayansi na Teknolojia mbeya(MUST) cha mkoani Mbeya huku akiwaacha watanzania wenye sifa ya kusimamia nafasi hiyo.
          
         Wachambuzi wa siasa wanasema anachokitetea rais_urundikaji madaraka mengi kwa mtu mmoja si utamaduni mzuri hata kidogo kwa kigezo chochote kile,Nchi inao watu wenye uzoefu na waliobobea kwenye nafasi hiyo.
         


        Swali la kujiuliza je tutalajie nini katika Taifa hili kwa viongozi wenye Nafasi zaidi ya moja ya uongozi,huku nafasi hizo ni nafasi kubwa katika ufanyaji wa Kazi,hivi leo hao wakuu wa mikoa na wa wilaya wako Dodoma je wanajua kinachoendelea kwenye mkio yao?

          Je kama Rais Kikwete alikosa watu wenye Sifa katika kuongoza nafasi hizo kulikuwa na Ulazima gan kuteua hao wakuu wa wilaya huku akijua wananafasi zengine?na kwanini asingeaacha nafasi hizo wazi au lengo lake lilikuwa kuwatajilisha makada wenzake kwa utajili kutokana na mtu mmoja kuwa na kazi zaidi ya mbili.

Tafakari

No comments: