=
Ofisa Masoko Mwandamizi Access Bank,
Muganyizi Bisheko (kulia) akimkabidhi moja ya kompyuta Mkuu wa Shule ya
Sekondari Azania, Mwl. Benald Ngonzie (kushoto), wanaoshuhudia
makabidhiano hayo ni wanafunzi wa shule hiyo. Benki hiyo jana ilitoa
msaada wa kompyuta 10 kwa shule hiyo zenye thamani ya zaidi ya Sh2
milioni.
Ofisa Masoko Mwandamizi Access Bank,
Muganyizi Bisheko (kulia) akimkabidhi moja ya kompyuta kwa wanafunzi
waliowawakilisha wenzao, anayeshuhudia makabidhiano hayo ni Mkuu wa
Shule hiyo, Mwl. Benald Ngonzie. Benki hiyo jana ilitoa msaada wa
kompyuta 10 kwa shule hiyo zenye thamani ya zaidi ya Sh2 milioni.
Ofisa Masoko Mwandamizi Access
Bank, Muganyizi Bisheko (kulia) akimkabidhi moja ya kompyuta makamu wa
rais wa shule ya sekondari ya Azania, Johnson Kaaya, wanaoshuhudia
makabidhiano hayo ni Mkuu wa shule hiyo, Mwl. Benald Ngonzie. Benki hiyo
jana ilitoa msaada wa kompyuta 10 kwa shule hiyo zenye thamani ya zaidi
ya Sh2 milioni.
Mkuu wa shule ya Sekondari ya
Azania, Mwl. Benald Ngonzie akiongea na wanafunzi mara baada ya
makabidhiano ya kompyuta kwa shule hiyo iliyotolewa na Access Bank.
Benki hiyo jana ilitoa msaada wa kompyuta 10 kwa shule hiyo zenye
thamani ya zaidi ya Sh2 milioni.
Ofisa Masoko Mwandamizi Access Bank,
Muganyizi Bisheko akiongea na vyombo vya habari mara baada ya kukabidhi
kompyuta kwa shule hiyo. Picha zote na Cathbert Kajuna wa Kajunason
Blog.
—
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam.
Shule ya sekondari ya Azania
inakabiliwa na uchakavu wa miundombinu ikiwamo majengo na ubovu wa vyoo,
hali inayohatarisha afya za wanafunzi hao kutokana na kuwapo kwa
majimaji anayoweza kuzalisha mbu waenezao ugonjwa wa Malaria na Dengue.
Akizungumza jana baada ya kupokea
msaada wa kompyuta 10 kutoka katika benki ya Access, Makamu Mkuu wa
shule hiyo Elizabeth Ngoda alisema shule hiyo ni kongwe kwa sasa
kutokana na kujengwa muda mrefu hivyo inahitajika ukarabati wa kina.
“Shule ni kongwe na imezalisha
viongozi mbalimbali na sasa imechakaa, majengo yanahitajikukarabatiwa na
vyoo havitoshi, lakini tunawashukuru Access Bank kwa kutuletea kompyuta
hizi, kwani tulikuwa na kompyuta 25 awali ambazo hazikukidhi mahitaji
kutokana na kuwa na idadi kubwa ya wanafunzi,” alisema Ngoda na
kubainisha kwamba shule ina wanafunzi 2000 na wafanyakazi 115.
Ngoda alitoa wito kwa wadau wengine
pamoja na wanafunzi waliowahi kusoma katika shule hiyo,kujitolea kwa
hali na mali ili kuirudisha Azania katika hali nzuri ya kimazingira.
Makamu wa rais wa shule hiyo Johnson
Kaaya aliwashukuru wadau hao huku akitoa wito kwa makampuni mengine
kuchangia katika kurekebisha kasoro kadhaa zilizopo shuleni hapo hasa
miundombinu.
“Tunaahidi kuzitumia kompyuta hizi
katika kuleta ufanisi na si vinginevyo, tunaomba hii iwe chachu kwa
makampuni mengine kusaidia zaidi kwani changamoto kubwa hapa shuleni
kwetu ni uchakavu wa majengo, hatuna viti, vyoo vibovu na pia tunapata
taabu kipindi cha joto kwani hakuna feni,” alisema Kaaya.
Naye Ofisa Masoko Mwandamizi wa
Access Bank, Muganyizi Bisheko alisema msaada huo ni katika mwendelezo
wa mchakato wa kusaidia sekta ya elimu nchini hasa katika upane wa
teknolojia ya abari na mawasiliano ambayo imeonekana kuwa kikwazo
kikubwa katika utafutaji wa ajira kwa vijana ambao humaliza shule bila
kuwa na utaalamu wa kompyuta.
“Tunaamini kupitia kompyuta hizi
wanafunzi wataweza kujifunza programu mbalimbali ambazo zitawasaidia
katika kukuza elimu yao hapa shuleni na katika maisha yao,” alisema
Bisheko.
No comments:
Post a Comment