Katibu
Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasili katika
shule ya sekondari ya Kiwele kata ya Kitunda wilayani Sikonge mkoa wa
Tabora ambapo amekagua miradi mbalimbali ya nyumba ya walimu na maabara
zinazojengwa katika shule hiyo, Kinana akiongozana na Nape Nnauye Katibu
wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi pia amekagua majengo ya kituo cha afya
cha Kitunda, katika ziara hiyo mganga mkuu wa kituo hicho Dk.Silvanus
Kabutula amelalamikia kuchelew kwa ujenzi wa jengo la upasuaji na
kujifungulia akina mama wajawazito jambo ambalo linasababisha matatizo
makubwa kwa wakati wa kata hiyo na vijiji vya jirani ambavyo vinategemea
huduma kutoka katika kituo hicho, Akitolea ufafanuzi zaidi kuhusu suala
hilo mbunge wa jimbo la Sikonge Mh. Said Mkumba amesema, mkandarasi wa
ujenzi wa vituo hivyo ameshindwa kumaliza kazi kwa wakati na mkataba
ulianza 28/ 10/2009 na ulitakiwa kumalizika 2/5/2011 lakini mpaka sasa
vituo hivyo na zahanati havijakamilika jambo ambalo linakwamisha ustawi
wa jamii katika suala zima la afya, Ameongeza kuwa kupitia mradi wa
Mradi wa kupunguza vifo kwa akina mama Support to Martenal Mortality
Project Reduction (SMMRP)
jumla ya vituo saba vya kutolea huduma wilayani Sikonge vilitakiwa
kujengwa ambavyo ni Kipili,Kitumbi,Tumbili, Pangale,Kitunda, Mazinge na
Kisanga ambapo jumla ya shilingi bilioni 2,051,723,850 zimelipwa kwa
mkandarasi huyo hata hivyo kazi hiyo jaijakamilika mpaka sasa, Kuhusu za
la Tumbaku Mkumba amesema wakulima wa tumbaku waruhusiwe kuuza tumbaku
wanapotaka kwa sababu vyama vya ushirika vya msingi vinawadhulumu
wakulima hao. Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ameahidi
kufikisha kwa suala hilo kwa Mh. Rais Dr. Jakaya Mrisho Kikwete kilio
cha wananchi wa Sikonge kuhusu suala la zahanati hizo kutokumalizika
kwa wakati na matatizo ya wakulima kutolipwa fedha zao za mauzo ya
tumbaku kwa wakati.(PICHA NA FULLSHANGwe
Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi akiwasili katika shule hiyo. Katibu
Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akikagua moja ya
nyumba za walimu katika shule ya sekondari ya kiwele Kitunda. Katibu
Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akisaini kitabi
wakati alipowasili katika kituo cha afya cha Kitunda, Kushoto ni Mganga
mfawidhi wa kitu hicho Dk. Silvanus Kabutula. Katibu
Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akiaikiliza
taarifa ya mganga mfawidhiwa kituo cha afya cha Kitunda Dk. Silvanus
Katubula Katibu
Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akikagua kituo cha
afya cha Kitunda huku akongozana na Mh. Said Mkumba mbunge wa jimbo la
Sikonge. Katibu
Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akiongozana na
mganga mfawidhi wa kituo cha afya cha Kitunda wakati akikagua miradi ya
maendeleo katika kituo hicho, kulia ni Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi
Siasa na Uenezi. Katibu
Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akimsiiliza mganga
mfawidhi wa kituo cha afya cha Kitunda Sikonge wakati alipotembelea
kituo hicho kutoka kulia ni Mh. Said Mkumba mbunge wa jimbo la Sikonge
na anayefuata ni Nape Nnauye. Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasili katika eneo la mkutano wa hadhara kata ya Kitunda. Kwaya ikitumbuiza katika mkutano huo. Kikundi cha ngoma kikitumbuiza katika mkutano huo. Mkuu
wa mkoa wa Tabora Bi. Fatma Mwassa akimueleza jambo Katibu Mkuu wa
Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana wakati wa mkutano huo ,
kushoto ni Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi na
aliyesimama nyuma ni mbunge wa jimbo la Sikonge Mh. Said Mkumba. Kikundi cha kwaya ya Kitunda kikitumbuiza katika mkutano wa hadhara. Mkuu wa mkoa wa Tabora Bi. Fatma Mwassa akizungumza na wananchi wa kata ya Kitunda kuhusu zao la Tumbaku Mbunge wa jimbo la Sikonge Mh. Said Mkumba akizungumza na wananchi wa kata ya Kitunda Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi akizungumza na wananchi wa kata ya Kitunda katika mkutano wa hadhara. Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutunia wananchi wa kata ya Kitunda. Juma
Bakari Kaseka Mkulima wa tumbaku kata ya Kitunda wilayani Sikonge
akizungumza katika mkutano wa hadhara na kutoa malalamiko ya wakulia kwa
jinsi wanavyoibiwa fedha zao za mauzo ya Tumbaku. Bw.
Lameck Mnyama mkulima na Mjumbe wa mkutano mkuu wa Chama Kikuu cha
Ushirika wa wakulima wa tumbaku (WETCO)akilalamikia jinsi wakulima
wanavyodhulumiwa huku akionekana kuchoka kabisa wakati akielezea wizi
unaoendelea kwa wakulima wa tumbaku wakati wa malipo ya mauzo ya tumbaku
yao jambo ambalo linapoteza imani yake kwa chama hicho pamoja na kwamba
yeye ni mmoja wa viongozi wa (WETCO)
No comments:
Post a Comment