Mkurugenzi mtendaji wa AzamTV, bwana Rhys Torrington |
AzamTV leo wamezindua mashindano
yatakayowahusisha wapenzi wa kandanda yatakayojulikana kama KWETU HOUSE.
Mashindano haya ambayo ni mara ya kwanza Tanzania yatashirikisha wapenzi
na mashabiki wa mpira wa miguu ambapo watu kumi wa 10 wa timu mbalimbali
watachaguliwa na kuishi katika nyumba moja kwa muda wa siku 30 wakionyesha ni
jinsi gani wao ni mashabiki namba mmoja kwa timu zao .
Akizindua mashindano hayo, Mkurugenzi
mtendaji wa AzamTV, bwana Rhys Torrington alisema: Lengo kuu la kufanya
shindano hili ni kuamsha hisia za mashabiki wa soka na kuonyesha umuhimu wa
kuthamini mashabiki kwa sababu bila wao mpira wa miguu usingekuwepo leo hii; wakati
huo huo ni kuwaletea watazamaji vipindi vinavyoburudisha na kuelimisha.
Mashindano haya yametokana na
ubunifu wa wafanyakazi wa Azamtv ambapo hiki ni kipindi kimojawapo
kitakachofuatiwa na vingine vingi ambavyo viko ndani ya maandalizi kupitia
kampuni ya Uhai Production ambayo ni kampuni mama ya AzamTV; aliongeza bwana
Wasiwasi Mwabulambo ambaye ni mratibu wa mashindano hayo.
Mratibu wa shindano hilo wasiwasi mwabulambo akizindua rasmi |
Wanaoruhusiwa kushiriki mashindano
haya ni wanaume wenye umri wa miaka kumi na nane (18) na kuendelea.
Wakiwa ndani ya jumba la KWETU HOUSE
washiriki wataenguliwa kila siku ya jumapili mpaka kubakia washiriki watatu
ambapo mmoja wao atajinyakulia kitita cha shilingi milioni kumi (10)
Usaili wa shindano hili utafanyika
siku ya jumamosi tarehe 24/05/2014 uwanja wa Leaders club, kuanzia
saa 3 asubuhi hadi saa 11 jioni. Usaili utakuwa ni bure.
Pia mashabiki wanaweza kujisajili
kwa kutuma video zao fupi kwenda kwenye whatsApp number 0759 38
65 68 nakuonyesha ushabiki wao wa dhati.
Watakaochaguliwa watatangazwa tarehe
27/05/2014 ambapo wataingia ndani ya jumba la KWETU HOUSE tarehe 30/05/2014; na
mshindi atapatikana tarehe 27/06/2014.
Shindano hili limedhaminiwa na Azam
Energy Drink kwa ushirikiano wa Channel Ten, Magic Fm na Times Fm.
No comments:
Post a Comment