Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es
Salaam limeanza kufanya uchunguzi wa kina kuhusu sababu za kifo cha bwana
JULIUS S/O NITANGA @ GASHAZA , miaka 51,
Meneja Biashara wa EWURA, Mkazi wa YOMBO VITUKA (Jet- Rumo). Afisa huyo
alikutwa amefariki tarehe 18/05/2014, Kata ya YOMBO VITUKA, (M) Ilala katika
nyumba ya kulala wageni iitwayo MWANGA LODGE katika chumba Na: 133 katika hali
ambayo inaashiria kujinyonga kwa kutumia tai aliyokuwa ameivaa mwenyewe.
Licha
ya maelezo hayo, Jeshi la Polisi Kanda Maalum linafanya uchunguzi ili kuondoa
utata ulioanza kujitokeza kuhusu kifo hicho hasa baada ya tarifa kuanza
kuzagaa kwamba kifo chake kilitokana na
kutoelewana na viongozi wenzake katika masuala ya kikazi. Kinachofanyika ni
kupata maelezo ya kina kuhusu mwenendo wa shughuli za marehemu na hali
iliyomsibu kabla ya kifo chake kwani marehemu hakuacha ujumbe wowote aidha wa
maandishi au wa mdomo.
Aidha,
Kamishna wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaa ameunda jopo la wapelelezi
likiongozwa na Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalum D’Salaam akishirikiana na
wataalam wa Maabara Kuu ya Polisi (Forensic Bureau) katika kufanya uchunguzi wa
kina kuhusiana na tukio hilo. Aidha maelezo mbali mbali ya mashahidi
yanaendelea kuchukuliwa ili kujua kama kuna kosa la kijinai, kiutawala au
yote.
Taarifa kamili ya mwelekeo wa
shauri hili itatolewa hivi karibuni.
MAJAMBAZI
WAWILI WALIOKUWA WANATAFUTWA WAKAMATWA WAKIMILIKI BASTOLA.
STORY NYINGINE KALI TOKA KWA KAMISHNA KOVA BOFYA CHINI
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es
Salaam limewakamata majambazi wawili huko KIWALANI MINAZI MIREFU, (M) Ilala
wakiwa na Bastola moja aina ya STAR LANCER yenye namba SA CAL 22LR HK 708022
ikiwa na risasi moja ndani ya Magazine. Walipohojiwa walikiri kuhusika katika
matukio kadhaa ya ujambazi na waliwataja wenzao ambao wamekuwa wakishirikiana
nao katika matukio mbalimbali.
Majambazi
hao waliokamatwa na silaha ni
·
ALLY
S/O JUMA ALLY @ LIKWALE
·
CHARLES
S/O CHIGANGA MALIMA @ PASTOR, miaka 32, mkazi wa
Tandale Uzuri.
Aidha,
watuhumiwa waliotajwa kushirikiana na watuhumiwa hao wanasakwa kwa mbinu zote
waweze kuwaonganisha na wenzao ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao.
KUKAMATWA
NA MALI ISAFIRISHWAYO KWENDA NCHI JIRANI YA BURUNDIDRC PAMOJA NA WATUHUMIWA
WATATU.
Mnamo tarehe 18/05/2014 Jeshi la
Polisi Kanda Maalum lilipokea taarifa kutoka
kwa msiri kuwa kuna gari lenye Na. T.649 BAY mali ya RUOTA INVESTIMENT limepakia
mali iliyokuwa inasafirishwa kwenda nchini BUJUMBURA-BURUNDI kutoka kiwanda cha
MURZAH OIL kwamba mali hiyo inashushwa huko Sinza Afrika Sana.
Polisi
walichukua hatua za haraka na kufika eneo la tukio na kukuta mali hiyo
inashushwa kutoka katika lori hilo na kupakiwa kwenye gari namba T.571 APH aina
ya Honda kwa ajili ya kubeba mzigo huo wa sabuni za unga aina ya Pulf na
T-issue.
Walipohojiwa
wahusika kama mwenye mali ana taarifa juu ya kushushwa kwa mali hiyo
walishindwa kutoa maelezo yanayoeleweka. Taratibu za kisheria zilifuatwa na
watuhumiwa watatu wamekamatwa kwenye eneo la tukio ambapo walimtaja mtu mmoja
aitwaye TAIRO S/O? kuhusika na tuhuma za mizigo hiyo.
Inasemekana
mali hiyo ina thamani ya Tshs 70,000,000/= (Shilingi Millioni Sabini) za
kitanzania ambapo mali yote imeokolewa na Polisi inamtafuta mmiliki wa mali
hiyo ili kuungana nae kukamilisha upelelezi wa shauri hilo.
Watuhumiwa
waliokamatwa kuhusiana na tukio hili ni
·
MWARABU
S/O HAKIKA, Miaka 23, Mfanyabiashara, Mkazi wa kijitonyama.
·
IDD
S/O JASINA, Miaka 48, Mfanyabiashara, Mkazi wa Kijitonyama.
·
RASHIDI
S/O SAID, Miaka 17, Mkazi wa Kijitonyama.
KUKAMATWA
KWA MAGARI SITA YA WIZI
Mnamo tarehe 05/05/2014, Kikosi Maalum
cha Kuzuia na Kupambana na wizi wa
magari kiliendesha oparesheni maalum katika jiji la Mwanza kwa kushirikiana na
kikosi kazi cha Polisi Mwanza kuyatafuta magari kadhaa yaliyoibwa jijini Dar es
Salaam katika matukio tofauti na siku tofauti. Hii ni baada ya Jeshi la Polisi
Kanda Maalum Dar es Salaam kupokea taarifa toka kwa wasamalia wema kisha kutuma
kikosi hicho kwenda jijini Mwanza.
Katika
oparesheni hiyo yalipatikana magari sita aina mbamlimbali kama ifuatavyo:
·
Tarehe
06/05/2014, huko maeneo ya Nyakato Buzuruga ilikamatwa gari namba T.154 CRH,
T/Mark II “Grande”, rangi “Pearl White” ikiendeshwa na GEOFREY S/O ISAKA CHABA, Miaka 45,
Mfanyabiashara, Mkazi wa Nyamanoro jijini Mwanza, aliyedai kuuziwa gari hilo na
dalali YUSUFU S/O CHACHA, mkazi wa Mwanza. Gari hili inasemekana ni mali ya
AIDA D/O AUGUSTINO HAULE, Miaka 35,
Mfanyabiashara, Mkazi wa Yombo Vituka jijini Dar es Salaam.
·
Tarehe
07/05/2014, maeneo ya Nyakato jijini Mwanza, ilikamatwa gari namba T.438 CKP, T/VEROSA,
rangi “Pearl White”, ikiendeshwa na SHABAN S/O SALUM MGONJA, Miaka 24,
Mfanyabiashara, Mkazi wa Nyakato Sokoni aliyedai kuuziwa gari hilo na Mchungaji YUSUPH S/O ERNEST BUJIKU
wa Kanisa la PENTEKOSTAl BUZURUGA jijini Mwanza. Gari hili liibiwa Yombo Vituka
nyumbani kwa REHEMA D/O SAIDI ILUNGA, miaka 30, Mfanyabiashara.
·
Tarehe
08/05/2014, maeneo ya CAPRIPOINT karibu na Hotel ya Tilapia ilikamatwa gari
namba T.787 BRW, T/CARINA SI, rangi ya Silver ikiwa imetelekezwa baada ya
dereva kuona msako umekuwa mkali sana. Upelelezi wa awali unaonyesha gari hili
liibwa huko Kinondoni ambalo mmiliki
wake ni AMANI S/O ABDALLAH MLILAPI wa jijini Dar es Salaam.
·
Aidha,
tarehe 11/05/2014, maeneo ya katikati ya Jiji la Mwanza ilikamatwa gari namba
T.895 CTU, T/Cresta GX 100, rangi ya Silver, ikiendeshwa na GODWIN S/O SHARTIEL
KWEKA, miaka 28, mkazi wa Nyakato jijini Mwanza. Alieleza kuuziwa gari hilo na FIDELIS
S/O LAURENCE KIMBAGE, miaka 36, mkazi wa Nyakato – jijini Mwanza. Gari hili
liibiwa maeneo ya Kinyerezi Bonyokwa nyumbani kwa VICTOR S/O BENSON USUMA, miaka 29, mfanyabiashara.
·
Pia,
tarehe 14/05/2014, huko Mkoani Geita kwenye machimbo ya madini ya GEITA GOLD
MINE lilikamatwa gari namba T.891 BFF, T/NOAH, Rangi Nyeupe, ikiendeshwa na
VENANCE S/O BUKUKU, miaka 30, mfanyabiashara. Gari hilo liibiwa huko YOMBO BUZA
nyumbani kwa SALUM S/O MWISHEHE KULITA, miaka 32, Afisa wa Bank ya NMB Makao
Makuu.
·
Tarehe
04/05/2014 huko Morogoro, lilikamatwa gari namba T.570 BZX, T/NOAH, rangi ya
Silver, ikiendeshwa na HUSSEIN S/O ALFAN SAID @ MASOFA, miaka35,
Mfanyabiashara, mkazi wa Morogoro. Alipohojiwa alidai kuuziwa gari hilo na
dalali SIWAMBALI S/O SAID MOHAMED. Gari hilo ni mali ya MOHAMED S/O GHALIB
MWARABU, miaka 42, mkazi wa Ilala.
KUKAMATWA
KWA MALI YADHANIWAYO KUWA YA WIZI
Jeshi
la Polisi Kanda Maalum D’Salaam huko maeneo ya Tabata Matumbi limefanikiwa
kukamata magari mawili yenye Namba T.539 BEX aina ya Mitsubish Canter rangi ya
blue ikiwa imebeba mabox 180 ya misumari, na T.377 CME Toyota Noah rangi nyeupe
likiwa limebeba mabox 42 ya balbu mali idhaniwayo kuwa ya wizi pamoja na
watuhumiwa 3.
Hii
ni baada ya Polisi waliokuwa doria kuyatilia mashaka magari hayo.
POLISI
WAZIDISHA MAPAMBANO DHIDI YA KERO YA FOLENI JIJINI D’SALAAM
Jeshi
la Polisi Kanda Maalum D’Salaam limeamua kutumia mbinu mbali mbali mbadala ili
kupambana kikamilifu na kero ya foleni inayowakabili madereva wa magari au
vyombo vya moto jijini D’Salaam. Mbinu
hizo za kukabiliana na foleni ni pamoja na kuongeza idadi kubwa zaidi ya askari
wa Jeshi la Polisi ambao watatanda katika barabara Kuu zinazoingiza magari
mengi katikati ya Jiji wakati wa asubuhi na hatimaye wakati wa jioni, magari
hayo na kwa wakati mmoja kutoka katikati ya jiji. Mtandao huo mkubwa wa askari wa doria utaanza
kazi kuanzia saa 10 alfajiri hadi saa 5 usiku wakati msongamano huo wa magari unapokuwa
umepungua. Askari hawa wa Usalama
Barabarani na wengine kutoka vikosi mbali mbali watafanya kazi katika mtindo wa
kupokezana (shift) ili kuleta ufanisi na ubora wa kazi. Mtindo huu utawabana watumiaji wa barabara
wenye mtindo wa kutanua ambao watakamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria papo
kwa papo (notification fines) au kufikishwa mahakamani bila msamaha au visingizio
vyovyote.
Aidha
uwepo wa askari hao kwa wingi barabarani utapunguza makosa ya usalama
yanayofanywa kwa makusudi na wenye magari aua pikipiki ambao wengine hawajali
ishara za taa za usalama barabarani (traffic lights), uchomekeaji usiozingatia
taratibu za kiusalama, mwendo kasi, kuongea na simu za mkononi wakati dereva
akiendesha gari, kutofunga mikanda ya dereva au abiria. Aidha zoezi hili litaenda sambamba na ukaguzi
wa uzima wa magari, kutokuwa na bima, leseni ya barabara (Road Licence) na
uchakavu wa gari au pikipiki kwa ujumla.
Sambamba na zoezi hili tunaomba madereva raia wema watakaogundua
madereva wanaofanya makosa ya makusudi mbele, nyuma au pembeni watoe taarifa
Polisi kwa namba zifuatazo:-
1.0732
-928728 - USALAMA BARABARANI KANDA MAALUM
2.0713-224848
- MKUU WA USALAMA BARABARANI KANDA
MAALUM
3.0787
– 668306 – AU 022-2138177 – KIKOSI CHA 999
NAMBA ZINGINE NI ZA WAKUU WA USALAMA BARABARANI
MIKOA YA:
4.0713
– 207090 - KINONDONI
5.0655
– 678260 - ILALA
6.0658
– 376477 - TEMEKE
Tahadhari
inachukuliwa kwamba zoezi hili lina lengo la kuboresha kazi za Polisi na kuleta
huduma bora kwa watumiaji wote wa barabara na kuondoa adha kubwa ya foleni
yenye kuleta madhara ya kiuchumi na kijamii.
S.H. KOVA
KAMISHNA WA POLISI KANDA MAALUM
DAR ES SALAAM
No comments:
Post a Comment