Kamishna kova leo alipoamua kuitoa hadharani picha ya mtuhumiwa huyo mbele ya wanahabari ili apatikane mara moja |
Jeshi la Polisi Kanda Maalum
D’Salaam limefanikiwa kumbaini mtuhumiwa mhimu ambaye ni kinara wa mtandao wa wizi
katika mabenki ambaye anajulikana kwa jina la RONALD S/O MOLLEL umri miaka 37,
mfanyabishara na mkazi wa Kimara Bonyokwa Jijini D’salaam.
Mtuhumiwa huyu amekimbilia mafichoni
mara baada ya tukio la ujambazi katika Tawi la Benki ya Barclays Kinondoni lililotokea tarehe 15/4/2014 ambapo
majambazi walifanikiwa kupora kiasi kikubwa cha fedha T.Shs.390,220,000/= , USD 55,000/= na EURO 2150/=. Aidha sasa imefahamika kwamba mtuhumiwa huyu
ni mume wa mtuhumiwa wa kwanza katika tukio la Barclays Benki aitwaye ALUNE D/O
KASILILIKA @ ALUNE D/O MOLLEL , miaka 28,
Mkazi wa Kimara Bonyokwa ambaye ni Meneja wa Benki Tawi la Barclays
Kinondoni. Mtuhumiwa Mollel anatafutwa
kwa kila hali kwa vile yeye ndiye alikuwa kinara wa kupanga tukio hilo la
Barclays na mara baada ya tukio ametoroka na kiasi kikubwa cha fedha hizo
zilizoibiwa.
RONALD S/O MOLLEL ambaye ndiye mtuhumiwa wa ujambazi katika mabenk mbalimbali hapa jijini dar es salaam |
Zipo taarifa za
kuaminika kuwa mtuhumiwa huyu amekuwa akipanga na kushiriki kikamilifu katika
matukio mbali mbali ya uhalifu mkubwa ikiwa ni pamoja na kuongoza vikundi vya
majambazi vilivyowahi kupora katika mabenki mbali mbali katika kipindi cha
mwaka mmoja uliopita. Mtuhumiwa huyo ni
hatari kwani ana mtandao na watumishi muhimu katika matawi mbali mbali ya
mabenki kwa lengo la kufanikisha uhalifu katika mabenki hayo.
Endapo utamona mtu huyu toa ripot mahali popote hata kwa mmiliki wa blog hii |
Jeshi la Polisi limelazimika
kutoa picha yake hadharani kwa kutumia dhana ya ulinzi shirikishi ili mtuhumiwa
huyu akionekana akamatwe na taarifa zitolewe katika kituo chochote cha Polisi
ikiwa ni lengo la polisi kupambana na uhalifu katika dhamira ya kuzuia uhalifu,
kulinda maisha na mali za wananchi.
Zawadi nono ya fedha taslim itatolewa kwa siri kwa mtu yeyote atakayetoa
taarifa zitakazosaidia kukamatwa kwa mtuhumiwa huyu. Pamoja na maelezo hayo mtuhumiwa mwenyewe
sasa anapewa fulsa ya kujisalimisha katika kituo chochote cha polisi kabla ya
kukamatwa kwa njia nyingine.
No comments:
Post a Comment