Tuesday, May 20, 2014

SAKATA LA NYALANDU SASA LAFIKIA PATAMU,IKILU YASALIMU AMRI KWA NYALANDU

      Na Karoli Vinsent
               
        IKULU  ya Rais Jakaya Kikwete Imezidiwa Nguvu na Waziri wa Maliasili na Utalii,Lazaro Nyalandu,baada Ikulu hiyo kusalimu amri kwa Waziri huyo kutokana na Kitendo cha ikulu kuwaondoa kwenye Nyadhifa zao Wakurugenzi wa Wanyama Poli,Profesa Alex Songorwa na Japhari Kidegesho.
           
          Kuzidiwa, nguvu  huku kwa Ikulu ya Rais kumetokanaTaarifa za awali,ambazo katibu Mkuu Kiongozi,Balozi Ombene Sefue alipopuuza uamuizi wa Waziri Nyalandu na kuwarudisha kazini Wakurugenzi hawo baada ya Kutimuliwa na Waziri huyo.


   Lakini, Baadae kutokana na Nguvu na Mikwara aliyokuwa anaitoa Waziri Nyalandu,kuhusu kuwarudisha Viongozi hao,ikaifanya  Ikulu ya Rais Kikwete Ikanywea na Kuwaondoa  katika Nyadhifa hizo.

     Kwa Mujibu ya Vyanzo kutoka ndani ya Ikulu,vilivyozungumza na Mwandishi wa Mtandao  ambao hawakutaka Majina yao kutajwa kwenye Mtandao huu walinasema Waziri Nyalandu anambinu Nyingi sana katika kumshawishi hata Rais Kikwete.

  “Kiekweli ndugu Mwandishi hakuna wakuweza na kumpiku Nyalandu hata mimi mwenyewe sikutegemea kama ikulu itanywea Kiasi hichi na kuwaondoa wale wakurugenzi ,kwa hatua hii Nyarandu anageuza wizara kuwa sehemu yake ya kufanya anavyotaka,na sijui kwanini Rais Kikwete anashindwa hata Kumchukulia Hatua Nyalandu”kilisema Chanzo hicho.

          Nyalandu,ambae akekuwa akiandamwa na Vyombo mbalimbali vya Habari Ndani ya Nchi na Nje ya Nchi,kutokana na Kugeuza Wizara hiyo kuwa Genge la kufanya  Vitendo vyake vya Ufisadi.

         Duru za Mambo zinasema Ikulu ya Rais Kikwete Imebariki vitendo vya UJangili na Ufisadi Ndani ya Wizara hiyo ya Maliasili,kutokana na Kitendo chake kuwaondoa watu waliokuwa wakipambana na kuondoa Ujangili Nchini wakiwemo, Profesa Alex Songorwa na Japhari Kidegesho.

       Chanzo hicho kilisema Sakata hilo la Uongozi ndani ya Maliasili ,kilisema mabadiliko  hayo ya Gafla  yamefanywa siku chache tu baada ya Nyalandu kudaiwa kufika ikulu na kufanya mazungumzo na Balozi Sefue.

     Hii ilikuja Siku mbili baada ya Nyalandu kumtimua prof.songorwa kwenye Kikao cha Uongozi wa Wizara na Kamati ya kudumu ya Bunge ardhi,Maliasili na Mazingira inayoongozwa na James lembeli,Mbunge wa Kahama mkoani Shinyanga.

      Nyalandu,ambaye anatuhumiwa kutokana na Kitendo chake cha kufanya Jalibio la kuuza Hifadhi ya Taifa ya Katavi kwa kampuni ya Africa Parks Networks (APN) la nchini Afrika kusini.

    Mpango, huo wa kifisadi ulikuwa umesukwa na Waziri huyo na Mbunge wa Kahama,Jemes Lembeli,ambaye inasemekana ni mwenyekiti wa Bodi kampuni ya APN.

       Vilevile chanzo hicho kilihoji uhusiano wa karibu kati ya Waziri Nyalandu na Mbunge wa Kahama Jemes Lembeli,wakati ikisitishwa kwa oparesheni tokomeza ujangili kulikofuatiwa na hatua bunge kutaka kamati ya bunge ya Ardhi,Maliasili na mazingira inayoongozwa na Lembeli kuchunguza mwenendo wa Oparesheni hiyo.

Ndipo kamati hiyo ilonyesha udhaifu mkubwa kwa mkurugenzi wanyama pori,ambaye inasemekana  ni kikwazo kwa Lembeli katika kufanikisha mradi wake huu wakuuza Hifadhi.
Vitendo hivyo vya Kibabaishaji anavyifanya Waziri Nyalandu ndani ya Wizara hiyo ilizidi kuibuliwa wakati ilipokuwa inawasilishwa bajeti ya Kambi ya Upinzani Bungeni, wakati wa wizara ya Maliasili na Utalii ilivyokuwa ikiwasilishwa.

  
       Waziri Kivuli wa Maliasili na Utalii mchungaji Peter Msigwa alisema  vitendo vya Ujangili Vimekuwa vikifanywa na Vigogo kutoka ikulu ambao ni Marafiki zake Rais Jakaya kiwete

        Msigwa alisema,waandamizi hao ni maofisa usalama wa taifa, wanajeshi, wafanyabiashara wakubwa, polisi, wanasiasa, Ikulu na watumishi wa umma.
Alisema Serikali ya CCM imekuwa ikitoa kauli za kubeza pamoja na majibu mepesi ya tuhuma hizi, huku tatizo la ujangili likiendelea kulichafua taifa katika jumuia ya kimataifa.

        “Katika hali ya kushangaza, baada ya gazeti la Mail on Sunday la nchini Uingereza kutoa taarifa kuwa biashara ya ujangili inahusisha watu wa karibu na rais wakiwemo wanasiasa, maofisa wa serikali na wafanyabiashara wakubwa, serikali ilitoa matamko mbalimbali pamoja na kulaani taarifa ya gazeti hilo.

   “Hatimaye Waziri Lazaro Nyalandu alimwalika mwandishi wa gazeti hilo kujionea mwenyewe shughuli za serikali za kupambana na ujangili,” alisema.
Kwa mujibu wa Msigwa, mwandishi  pia alipewa fursa ya kutembelea ghala la kuhifadhia pembe za ndovu zilizokamatwa.

      Alisema mwaliko wake ulikuwa na lengo la kuthibitisha kuwa Serikali ya CCM haina la kuficha.

     “Lakini katika hali ya kushangaza, uchunguzi na taarifa zaidi umeonyesha kuwa ndani ya miaka minane, Serikali ya CCM imekuwa ikiomba kibali bila mafanikio kutoka CITES (Convention on International Trade on Endangered Species) cha kuuza shehena ya pembe za ndovu takribani 34,000 zenye uzito wa tani 125 zenye thamani ya dola za Kimarekani milioni 150, sawa na sh bilioni 244.5 za Kitanzania (kwa wastani wa sh 1,630 kwa dola 1),” alisema.
Mch. Msigwa alisema kuwa jumuia ya kimataifa imeshangazwa na kitendo cha Tanzania kuomba kibali cha kuuza shehena iliyokamatwa ya pembe za ndovu kwa kuwa ni biashara haramu, na kitendo cha serikali kuomba kuyauza ni sawa na kuchochea ujangili zaidi.

     Alisema kuwa kumekuwa na ongezeko kubwa la watu wanaojishughulisha na uwindaji na biashara ya nyara za serikali bila kibali au leseni toka mamlaka husika.

    Mbunge huyo alisema utafiti uliofanywa na Tanzania Wildlife Research Institute (Tawiri) katika mbuga ya hifadhi ya Selou na Mikumi, unaonyesha kuwa idadi ya tembo imeshuka kutoka 74,900 mwaka 2006 hadi kufikia 43,552 mwaka 2009.

    Alisema kuwa hali hiyo ina maana kwamba kwa kipindi cha miaka mitatu, takribani asilimia 42 ambayo ni tembo 31,348 katika hifadhi mbili tu waliuawa na majangili


No comments: