Na Karoli Vinsent
WAZIRI wa Uchukuzi Dk Harison Mwakyembe Ameingia kwenye Kasfa Nzito
,kutokana na Kitendo chake cha kushindwa kumchukulia hatua, Kaimu mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA),Mzee Maden Kipande,ambaye
amegeuza Mamlaka hiyo kuwa Genge la Ufisadi.
Dk Mwakyembe,ambaye anasifika kwa
Wananchi kutokana Uchapakazi wake na kutokuwa na Nidhamu ya Uwoga
asiyemwogopa mtu yeyote ,ambae atakuwa anavunja Sheria za Nchi alikuwa
anamwajibisha.
Lakini,mambo yamebadilika kwa Waziri
hiyo,ambapo sasa ameonekana ameshindwa kumchukulia hatua,Kaimu mkurugenzi wa
Mamlaka ya Bandari Kipande,kutokana na Vitendo vyake vya kifisadi.
Kwa Mujibu wa vyanzo vya kuaminika kutoka katika Mamlaka hiyo
ambayo ni kitovu cha Maendeleo ya Nchi yetu ambazo mwandishi wa mtandao huu
amezipata ,zinasema mkurugenzi huyo amekuwa akiwasimamisha wafanyakazi kinyume
na Taratibu na sheria.
Chanzo hicho kinasema mkurugenzi huyo,amekuwa akiwasimamisha watu tu
pasipo kuwa na kosa lolote kwa mfano mwishoni mwa mwezi uliopita ameanzisha
Mpango wa kumngoa Meneja wa Bandari ya Tanga,Hassani Kyomile eti akisema Meneja
huyo amekuwa akivujisha siri kwenye Gazeti moja la wiki akidai Mhariri wa
Gazeti hilo ni Mhaya ,na meneja huyo pia ni mhaya eti anavujisha siri kwenye
Gazeti hilo,ambapo kipande anaona kumfukuza meneja huyo kutarahisisha mipango
yake ya kifisadi pasipo kuvuja.
Chanzo hicho kilizidi kusema
Kipande amekuwa akijivunia kwa Wafanyakazi wake kwamba anaweza kufanya lolote
na hakuna wakumzuia,ambapo amesimamisha watu kazi zaidi ya miaka miwili huku
wakiwa wakipokea mishahara pamoja na malupulupu huku wakiwa nyumbani bila
hata ya kufanya kazi.
Chanzo hicho kiliwataja wafanya kazi
hao,miongoni mwao ni Mama Muhindi,ambaye alikuwa Mkurugenzi wa Masoko
TPA,ambaye alisimamishwa kazi na Kipande kwa Madai alikuwa anavujisha
siri(madudu)za TPA kuhusu kwenye vyombo vya Habari,licha ya mkurugenzi
kipande alishindwa kutokea wala kukanusha kwenye vyombo vya Habari juu ya
Ufisadi huo ,
Tuhuma,zingine zinazozidi kumkabili
kipande kuhatarisha usalama wa Bandarini kwa kutokuna na kutokuwepo na
Kamera CCTV pamoja na mita za kupima mafuta yanayoingia nchini kutokafanya kazi
kwa miaka mitatu sasa.
Jambo la kushangaza Mama huyo
Muhindi,alisimaishwa kazi tangu agosti 2013 na kipande,lakini hajahojiwa
wala kurudishwa kazini ,huku akizidi kuendelea kuchukua mshahara na Marupurupu
mengine bila kufanya kazi hadi sasa wala hajahojiwa na mamlaka yeyote.
Chanzo,hicho kilizidi kutaja orodha ya
Wafanyakazi walionewa na Kipande ambae ni Mfanyakazi mwingine ndugu
Msemo,aliyekuwa Afisa Ununuzi,naye alisimamishwa kazi tangu agosti2013 kwa
tuhuma zisizokuwa za Ukweli wowote, lakini mpaka sasa naye anaendelea kuchukua
mshahara pamoja na marupurupu yote pasipo kufanya kazi.
Waliosimamishwa na kipande kwa
tuhuma hewa
Hery Arika,aliyekuwa Men eja
Biashara wa Bandari ya Dar es Salaam,alihamishiwa makao makuu na kuambiwa
kuripoti idara ya utawala tangu April 2013 hadi leo hii,Analipwa mishahara na
marupurupu yake bila kufanya kazi kwa mwaka mmoja sasa,kwa madai ya Kipande
hamtaki.
Ajira za Upendeleo,
Kama kuna mgogoro unaofuka Moshi
Ndani ya Bandari basi ni huu unaotokana na Ajira za Mhandisi Alois
Matei,ambaye ni Naibu Mkurugenzi mkuu(Maendeleo ya Miundombinu)na mhandisi
William Shilla,ambaye ni mkurugezni wa Uhandisi.Taharifa zilizopo zinasema kuwa
Wahandisi hawa wawili waliajiriwa na Kipande kupitia Mlango wa Nyuma
,pasipo kufuata taratibu za sheria.
Huu ni Mwenderezo wa Unyama
unaofanywa na Kipande ndani ya Bandari pasipo kuchukuliwa Hatua yeyote kutoka
kwenye Taasisi za Kupambana na Rushwa TAKUKURU,wala Wizara husika ya Uchukuzi
ambao,mamlaka hiyo iko chini yake.
Huku,Kipande akinijinadi kwenye
mkutano na Uongozi wa mamlaka hiyo,akisema mtu yeyote atakaye pingana nae
anamngoa kwani yeye na mamlaka hiyo ya Bandari hawapati hasara yeyote bali
serikali ndio inapata hasara,na kama yuko mtu yeyeto atakaye pingana
naye(Kipande )basi atamfukuza Kazi.
Duru, hizo zinasema mzee Kipande
amekuwa akifanya Vitendo hivyo vya Kifisadi huku akijinadi Hakuna mtu wa
kumng”oa nafasi hiyo kwa Madai,eti anajuana Kigogo mmoja aliyoko Ikuru ya
Jakaya Kikwete,ambae amekuwa karibu na Kipande.Ndio maana Amekuwa akifanya
Vitendo hivyo akijua hakuna mtu wakumchukulia Hatua zozote.
No comments:
Post a Comment