WATANZANIA 14,000,000MIL HAWAJUI KUSOMA, KUANDIKA NA KUHESABU, UTAFITI WA EFAGMR

PROF. JUSTIANIAN GALABAWA AKIWASILISHA TAFITI ZA ELIMU KWA WOTE, KATIKA RIPOTI HIYO IMEONYESHA JUMLA YA WATANZANIA MILION 14 (33% OF 45MILION) HAWAJUI KUSOMA KUANDIKA NA KUHESABU. ILI KUNASUA TATITZO HILO SERIKALI LAZIMA IWEKE PESA KATIKA ELIMU
 Reporti ya elimu kwa wote iliyotolewa na education for all grobal monitoring repor(EFAGMR) iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu kubwa leo hii imetoka huku  repoti hiyo kibainisha  wazi kuwa jumla ya watanzania milioni 14 hapa  nchini hawajui kusoma, kuandika na kuhesabu.

Akisoma taarifa hiyo mbele ya waziri wa elimu na mafunzo ya Ufundi, Mh. Shukuru Kawambwa,Prof. Toka Chuo kikuu Cha Daresalam, Prof. Justianian Galabawa, amesema jumla ya watanzania milioni kumi na nne katika ardhi ya Tanzania hawajui kusoma, Kuandika, na kuhesabu.

Amesema, tafiti ambazo zimefanywa kwa vijana wa dalasa la tatu na la saba, wanafunzi wengi wa dalasa la tatu walishindwa kusoma na kuandika hata kuhesabu kwa masomo ya Dalasa la pili, hatua inayoonyesha wazi kuna tatizo kubwa katika kutoa elimu iliyo bora kwa Watoto wa Kitanzania,
waziri Kawambwa akifuatilia uwasilishwaji wa ripoti hiyo mapema hii le

Repoti hiyo imeenda mbele zaidi na kuonyesha ni watoto watatu tu ambao wanamaliza dalasa la saba wakiwa wanajua kusoma na kuandika miongoni mwa watoto 10 waliofanyiwa mihihati,

Akibainisha sababu ambazo zinachangia kwa kiasi kikubwa kwa watoto wa kitanzania kushindwa kusoma kuandika na kuhesabu ni kutokana na mazingira duni ya watoto wanayojifunzia, walimu wanaotumika kuwa na uwezo mdogo pamoja na madalasa yanayotumika kuwa na uwiano mbaya wa wanafunzi wanaotakiwa kuwa madasani,

Naye mwalimu wa shule ya wavulana ya Alhikima ya jijini Daresalaam, akitoa masikitiko yake mbele ya waziri, amesema kuwa watoto wengi wanafeli katika shule ni kutokana na walimu ambao wanaletwa katika mashule kutokuwa na uwezo unaostahili.

Mwalimu mkuu wa shule ya wavulana alhikima akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari, mwalimu alisema lazima serikali iwekeze kama inataka kukomboa elimu ya Tanzania
Amesema lazima serikali ikubali kuwekeza katika elimu kama kweli wanataka elimu bora kwa watoto wa kitanzania, vinginevyo tunajidanganya, kwani idadi ya watanzania ambao wanashindwa kusoma kuandika na kuhesabu itazidi kupanda kila mwaka,

Serikali iache ubahili katika suala la elimu, kama watakuwa tayari kuwekeza bila shaka tutapata elimu tunayoitaka na ya kiwango cha juu, viginevyo tunajidanganya wenywe, Alisema Bw. Swai.

Mpaka sasa mazingira ya elimu kwa kweli hayaridhishi, na ndio maana wanafunzi wengi ambao wanapata alama nzuri huko kidato cha sita wanakimbia fani ya ualium wakijua wazi kuwa haina faida kwao kwani kipato chake ni cha hali ya chini

WASHIRIKI WAKIFUATILIA KWA MAKINI RIPOTI HIYO YA ELIMU BORA KWA WOTE
Mwl. Anasema kama kweli tunataka kujinasua na elimu tulinayo sasa ni lazima tuanze kwa kuwekeza katika elimu ikiwemo na kuwavutia vijana wanaopata divion 1 kujiunga na ualimu wakiahidiwa maslahi mazuri na serikali kisha maslahi ya walimu yakaboresha, hapo tutaanza kuona elimu ikiboreka,

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.