Thursday, May 15, 2014

HEBU TAZAMA WATU WALIVYOMWAGWA DAMU PUANI KWENYE MKUTANO WA UKAWA MOROGORO, PICHA ZA TUKIO HIZI HAPA



Kijana mmoja amepigwakutoka kwa wafuasi wa Ukawa waliokuwa na mkutano mkoani Morogoro jioni hii baada ya kudaiwa kuwa miongoni mwa
waliomteka Mbunge Rose Kamli wakati wa uchaguzi mdogo jimboni Kalenga, mkoani Iringa.
 
Njemba huyo akipokea kichapo kutoka kwa wafuasi wa Ukawa mkoani Morogoro na baadaye kuokolewa na polisi.

 
Mwenyekiti wa Bavicha, John Heche akithibitisha kumtambua kijana huyo anayedaiwa kushiriki kumteka mbunge wao kwenye uchaguzi mdogo uliofanyika Jimbo la Kalenga, lringa.

Mmoja wa viongozi wa Chadema mkoa wa Morogoro, lnnocent Zawadi ambaye alikuwepo jimboni Kalenga naye akithibitihsa pia kumtambua kijana huyo.



Njemba huyo ambaye hakufahamika jina lake mara moja, aliangushiwa kipigo baada ya kuibuka na kuanza kumpiga picha Mwenyekiti wa Bavicha Taifa, John Heche. Baada ya kipigo cha nguvu, njemba huyo alinusuriwa na polisi waliomchukua kumtoa mikononi mwa wafuasi hao.
Mwenyekiti huyo wa Bavicha akithibitisha kumtambua kijana huyo anayedaiwa kushiriki kumteka mbunge wao kwenye uchaguzi mdogo uliofanyika Jimbo la Kalenga, lringa.

No comments: