.

UBALOZI WA PALESTINA NCHINI WALIA NA MAUAJI YANAYOFANYWA NA WAISRAEL NCHINI KWAO

Balozi wa palestina nchini Tanzania NASRI ABU JAISH akionyesha baadhi ya picha za mauaji yanayoendelea nchini kwao
Ubalozi wa palestina nchini Tanzania umeliomba baraza la usalama la umoja wa mataifa kutafuta suluhu ya mauaji yanayoendelea nchini palestina yanayofanywa na taifa la Israel  .
Akizungumza na wanahabari jijini dare s salaam balozi wa palestina nchini Tanzania NASRI ABU JAISH Amesema kuwa viteno vya mauaji vinavyoendelea nchini pallestina ni kinyume na haki za binadamu ukuzingatia kuwa vinawalenga wanawake na watoto na vinafanywa kwenye ardhi ya wapalestina.
Aidha balozi huyo ameongeza kuwa baraza la usalama la usalama la umoja wa mataifa limekuwa halitendi haki katika mikutano mbalimbali ya kuleta suluhu ya mgogoro huo kwani ni mgogoro wa muda mrefu na umekuwa ukikuwa kadiri siku zinavyoizidi kwenda.
Balozi huyo Amesema kuwa ubalozi wao unaamini kuwa nchi ya Tanzania ina nafasi kubwa katika kuwa suluhu ya mgogoro wao ikiwa ni pamoja na kuyashawishi mataifa mengine ya Africa kutafuta ufumbuzi wa mgogoro wao.
Katika mauaji yanayoendelea katika ardhi ya pelestina hasdi sasa wananchi 104 na wengine 600 wamejeruhiwa na wengi kati yao wakiwa ni watoto na wanawake.
Katika hatua nyingine balozi huyo amevishutumu vyombo vya habari vya magharibi kwa kuegemea upande mmoja wa Israel jambo linalopelekea kutopatikana kwa suluhu ya kudumu ya mgogoro huo


About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.