Friday, August 29, 2014

TIGO NA REACH FOR CHANGE WAZINDUA SHINDANO LA WAJASIRIAMALI JAMII,KILA MSHINDI KUJINYAKULIA DOLA 20,000

Meneja mkuu wa tigo Tanzania DIEGO GUTIEREZ  katikati akizungumza na wanahabari muda huu makao makuu ya tigo wakati akizindua rasmi shindano hilo kulia kwake ni meneja wa REACH FOR CHANGE Tanzania RICHARD GORVETT.
      Kampuni ya mawasiliano ya TIGO Tanzania kwa kushirikiana na shirika lisilo la kiserikali nchini la REACH  FOR  CHANGE leo wamezindua shindano la  wajasiriamali jamii  liitwalo TIGO DIGITAL CHANGE MAKERS lenye lengo la kuibua mawazo ua kibunifu ambayo yatasaidia kutatua matatizo yanayowakabili watoto na vijana nchini.

Meneja mkuu wa tigo DIEGO GUTIEREZ leo amezindua shindano hilo mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es salaam ambapo ametoa wito kwa watu kishiriki ili wajiwekee katika nafasi ya kushinda fedha taslim dola 20,000 ambazo kila mshindi atapewa azitumie katika utekelezaji wa mawazo yao ya kibunifu.
 Meneja  huyo alisema kuwa lengo lao ni kupata mawazo ya kibunifu ya kidigitali ambayo yataleta na kutatua matatizo yanayo wakabili watoto kwa kiwango kikubwa huku wakiendelea kuwekeza katika kukuza na kuimarisha huduma zao za mawasiliano katika maeneo yote nchini.

Mawazo yatakayowakilishwa katika shindano hili yanatakiwa kuonyesha uwezo wa kutumia simu kidigital teknologia ya habari na mawasiliano kuleta ufanisi na utekelezaji wa mawazo husika,ambapo amesema kuwa mtu anaweza kutuma mawazo yao kupitia www.tigo.co.tz/digitalchangemakers.

Kwa upande wake meneja wa nchi wa reach for change RICHARD GORVERT amesema kuwa licha ya kupata kitita cha dola 20,000 washindi pia watapewa vifaa vya kuendeleza utekezzaji wa mawazo yao ikiwa ni pamoja na kuapata ushauri kutoka kwa wafanyakazi waandamizi kutoka tigo na reach for change,aidha wataunganishwa na wajariamali wengine ambao tayari wamenufaika na mpango huo.
meneja wa nchi wa reach for change RICHARD GORVERT akizungumza na wanahabari
Mchakato huu wa kuwapata wajasiriamali jamii wa kidigitali  unaenda sambamba na na mkakati wa TIGO  wa kuendeleza maisha ya kidigital nchini.huu ni mwaka wa tatu mfululizo ambapo kampuni ya tigo na reach for change zimekuwa zikishirikiana kuwasaidia wajasiriamali jamii nchini ambapo jumla ya wajasiriamali 6 wamenufaika na mpango huo katika kipindi hiki ambao kwa pamoja na kupitia utekelezaji wa miradi yao wamewasaidia jumla ya watoto zaidi ya 5700 nchini.

No comments: