Friday, September 5, 2014

KAMISHINA KOVA AWATAKA MAAFISA NA ASKARI KUFANYA KAZI KWA WELEDI KWA KUFUATA MAADILI

Kamishna KOVA akiwa katika mkutano huo
Kamishna wa Polisi  Kanda Maalum Dar es salaam Suleiman Kova amewataka askari wote  wa Kanda hiyo  kufanyakazi kwa weledi, kuzingatia haki za binadamu, na kufuata maadili ya  kazi katika utendaji wao wa kila siku.

Kamishna Kova ameyasema hayo wakati akiongea na Maafisa na Wakaguzi katika kikao cha utendaji kilichofanyika katika ukumbi wa Bwalo la Maafisa Oysterbay, Kinondoni, jijini Dar es Salaam na kusisitiza  umuhimu wakutoa huduma bora kwa wateja kulingana na matarajio ya wananchi.


Aidha  Kamishna Kova amesisitiza usiri katika Taarifa zinazoletwa /zinazotolewa na wananchi na kwamba kwa kufanya hivyo  kutalifanya Jeshi la Polisi kuaminika kwa wananchi. Akizungumzia suara la rushwa, Kamishina Kova amewaasa askari kutojihusiasha  na kupokea rushwa kwani ni adui wa haki na kinyume na maadili ya kazi za Polisi.

Amehimiza ushirikishwaji wa wananchi katika kila hatua hasa katika mashauri mbalimbali ya kesi zao na kutenda kazi kwa uwazi hasa wakati wananchi wanapotakiwa kupata taarifa za mashauri yao au wanapoomba ushauri katika kero zinazowasibu.

Kila Afisa, Mkaguzi na askari lazima afanye kazi kwa bidii na ukakamavu ili mchango wa Jeshi la Polisi uonekane wazi kwa jamii ya watanzania na wageni wanaoingia na kutoka nchini pia wale wanaoishi nchini.


 

No comments: