Friday, September 5, 2014

samahani kwa picha inayotisha--AJALI MBAYA SANA IMETOKEA LEO MKOANI MARA,38 WAFARIKI HAPO HAPO,

 Kufuatia ajali mbaya iliyohusisha magari matatu wilayani Butiama mkoani Mara idadi ya watu waliopoteza maisha ni 38 hadi sasa huku majeruhi wakiwa ni 80.
   Kwa mujibu wa mkuu wa wilaya ya Butiama  Anjelina Mabula aliyezungumza na TBC muda mfupi uliopita ajali hiyo amesema ajali hiyo imehusisha basi la AM Coach lenye namba za usajili  T736 AWJ likitoka Musoma kwenda Mwanza limegongana uso kwa uso na basi T677 CYC J4 Express likitoka Mwanza kwenda Tarime na gari jingine dogo aina ya Nissan Corola P332 KKT likitoka eneo la Sabasaba yote yalikutana kwenye mteremko yakitokea juu kwenda Darajani katika kupishana hawakuweza kupishana yakagongana na wakati huo gari dogo likapaki pembeni nalo likagongwa kwa nyuma likasukumwa na kutumbukia mtoni.

Katika gari dogo kulikuwa na watu 8,wawili wamefariki dunia na majeruhi 36 kutoka kwenye mabasi nao wamefariki na majeruhi 80 wamekimbizwa katika hospitali ya mkoa wa Mara.

Madereva wote wamefariki dunia

HABARI24 BLOG imeambiwa kuwa ajali hiyo imetokea wakati gari aina ya landcruiser kuingia barabarani ghafla ,ndipo Bas la Mwanza Coach  likitoka Musoma kwenda Mwanza likaivaa gari hiyo na wakati huo huo basi  la J4 Express likitoka Mwanza  kwenda Tarime nalo likagonga magari hayo.

Ajali hii imetokea majira ya saa 5 na nusu ,Majeruhi wamekimbizwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mara

PICHA ZAIDI ZITAKUJIA

Taarifa hii ni kwa msaada wa malunde1

No comments: