SERIKALI nchini imesema ifikapo mwakani mwezi wa
kumi Hospitali zote za Rufaa nchini zitaunganishwa kwenye mkongo wa Taifa kwa
lengo la kuboresha huduma za afya nchini.
Hayo yamesemwa leo Jijini Dar Es Salaam na Waziri wa Sayansi na
Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa wakati akizindua huduma mpya na ya kisasa ya
Video ya mikutano,ambapo Profesa Mbarawa alisema Mkongo wa Taifa umekamilikia
kwa asilimia kubwa na kuongeza ifikapo mwakani watahakikisha hospitali zote nchini
zinaunganishwa kwenye mkongo wa taifa hili kuongeza ubunifu na uwajipikaji kwa
watendaji wa Afya.
Profesa
Mbarawa alizidi kusema nia ya Wizara yake ni kuifanya Sekta ya “Internet”Mtandao
Inakua kwa kasi hapa nchini na kuleta Tija katika Taifa huku ikizingatia Dunia kote sekta ya
Mawasiliano imekuwa muhimili wa uchumi.
Vilevile
Profesa Mbarawa alisema kwa kuzinduliwa kwa Huduma ya Video Mkutanoni
itapunguza gharama ilizokuwa inazipata Serikali kwa kutenga Fedha kwa Watendaji kusafiri kutoka mkoa mmoja hadi mkoa
mwingine kwa ajili ya Kikao lakini kwa mfumo huu mpya uliozinduliwa leo
utawaondolea Adha hiyo na kuwafanya watendaji wa mikoa na Wilaya kukaa walipo
na kutumia njia ya Video kuwasiliana na watendaji wengine pasipo kwenda kwenye
eneo la tukio.
Aidha, Profesa Mbarawa aliwataka watanzania kutumia mitandao ya Kijamii
kwa lengo ya kupata taarifa na kuongeza ujuzi wa mambo na kuacha tabia hasi ya
kutumia mitandao ya Jamii kuchafua watu na kuonyesha picha chafu.
Huduma ya Video ya Mkutanoni imeanza kwa Mikoa zaidi
ya mitano ambapo huduma hiyo itapunguza urasimu uliopo wa kutumia Fedha nyingi
za Serikali.
No comments:
Post a Comment