Monday, October 6, 2014

Menejiment ya NBC yakutana na Mheshimiwa Rais Ikulu leo.

Rais Jakaya Kikwete (kulia) akizungumza na Mtendaji Mkuu wa Menejiment ya Barclays Africa, Mizinga Melu  (wa tatu kushoto) alipokwenda kumuaga Ikulu, Dar es Salaam leo. Wengine kutoka kushoto ni Kaimu Mkuu wa Masoko na Mawasiliano, Rukia Mtingwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Muda wa NBC, Pius Tibazarwa. Bi Melu aliyekuwa mkurugenzi tendaji wa benki hiyo alichaguliwa kushika wadhifa huo hivi karibuni


Rais Jakaya Kikwete akishikana mikono na Kaimu Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa NBC, Rukia Mtingwa (kushoto) wakati  Mtendaji Mkuu wa Menejiment ya Barclays Africa, Mizinga Melu (wa pili kushoto) alipokwenda Ikulu, Dar es Salaam kumuaga mheshimiwa rais. Wengine ni Mkurugenzi Mtendaji wa Muda, Pius Tibazarwa na Meneja Mahusiano, William Kallaghe (kulia).



Rais Jakaya Kikwete akishikana mikono na Mkurugenzi Mtendaji wa Muda wa  NBC, Pius Tibazarwa (wa pili kulia) mara baada ya hafla hiyo. Wengine kutoka kushoto ni Kaimu Mkuu wa Masoko na Mawasiliano, Rukia Mtingwa, Mtendaji Mkuu wa Menejiment ya Barclays Africa, Mizinga Melu na  Meneja Mahusiano wa benki hiyo, William Kallaghe.


No comments: