Saturday, October 4, 2014

SHIRIKA LA AMREF SASA WAGUSWA NA MATATIZO YA UZAZI KWA WANAWAKE NCHINI,SOMA WALICHOTANGAZA KUFANYA HAPA

Mkurugenzi mkaazi wa shirika la AMREF Tanzania  FESTUS ILAKO akizungumza na waanahabari Jijini Dar es salaam kuhusu harambee hiyo
 Shirika lisilo la kiserikali Tanzania  AMREF linatarajia kufanya harambee ya kuchangisha fedha kwa ajili ya kusaidia huduma za uzazi kwa wanawake mnamo October 9 mwaka huu jijini Dar es salaam.
Akizungumza na wanahabari jijini M Dar es salaam mkurugenzi mkaazi wa shirika hilo FESTUS ILAKO amesema kuwa mpango huo umekuja kufwatia changamoto kubwa iliyoko kwenye secta ya uzazi kwa wanawake kwa sasa.

Bw ILAKO amesema kuna tatizo kubwa sana la uhaba wa wakunga hapa nchini hivyo amesema kuwa pesa ambazo zitapatikana zitasaidia kupeleka wanafunzi vyuoni kwa ajili ya kupewa mafunzo yanayohusiana na uzazi kwa wanawake.

Amesema kuwa idadi kubwa ya vifo vya wanawake na watoto wakati wa kujifungua imeongezeka hapa nchini kutokana na uhaba wa wataalam hivyo mpango huo utaleta ahueni kwani utazalisha wataalam wengi ambao watapelekwa katika maeneo mbalimbali hapa nchini.
Mkurugenzi mkaazi wa shirika hilo FESTUS ILAKO (katikati) akiwa na mwakilishi wa chama cha wakunga Tanzania Bi FEDDY MWANGA (kulia) pamoja na mwakilishi kutoka benk M ms JACQUELINE ambao nao wametoa mchango mkubwa katika kufanikisha jambo hili
 Kwa upande wake mwakilishi wa chama cha wakunga Tanzania Bi FEDDY MWANGA amewaomba watanzania kuwa mstari wa mbele katika kupmbana na matatizo ya akina mama kwana wanawake wana umuhimu mkubwa katika jamii ambapo pia amelipongeza shirika la AMREF kwa hatua waliyoiamua katika kuwasaidia wanawake wa Tanzania,huku akiisihi serikali nayo kuunga mkono jitihada hizo ili kufikia malengo.

No comments: