Thursday, November 6, 2014

HAWA NDIO WATANGAZAJI WALIOTAJWA KUTAKA KUTUMIWA NA IKULU KUURUBUNI MCHAKATO WA KATIBA

Na Karoli Vinsent

             KATIBU mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Dokta Wilbroad Slaa amefanikiwa kupata waraka kutoka ndani ya Ikulu ya Rais Jakaya Kikwete ambapo Waraka huo umetenga kiasi cha Sh Bilioni 2.5 kwa ajiri ya kuvionga vyombo vya Habari na waandishi na watangazaji ili kuipigia Kampeni Katiba ilyopendekezwa,
       
            Waraka huo ambao mtandao huu unao unawaonyesha watangazaji kutoka Tv mbalimbali nchini, ambao ikulu ya Rais Jakaya kikwete imepanga kuwanunu ili kufanya kazi ya kuongoza vipindi mbalimbali  nyenye lengo la kuwafosi wananchi waipigie kura ya ndio wakati wakuipigia kura katiba iliyopendezwa.
      
               Dokta Slaa aliufichua waraka huo juzi Jijini Dar Es Salaam wakati wa mkutano na waandishi wa Habari Jijini Dar Es Salaam ambapo Kwa mujibu wa Waraka huo kila mtangazaji wa kituo cha TV ambaye ataongoza kipindi kimoja atapewa kiasi cha sh laki mbili (200000) kwa kila kipindi ndani ya wiki 22 yaani katika wiki moja kipindi kitaruka mara mbili kwa wiki na wananchi wataruhusiwa kupiga simu.
       
            Waraka huo umewataja watangazaji wa vituo vya TV ambao watanunuliwa,Natha Chingu ambaye ni Msimamizi wa Vipindi wa redio ya East Afrika ambayo yeye atakuwa mtangazaji wakipindi cha Katiba ndani ya Runinga ya EATV pamoja Samson Charlses kutoka kituo cha Tv EATV,
       
           Kwa upande wa kituo cha Runinga cha ITV ni  watangazaji hao ni Abdallah Mwipaya,Fatuma Shangasa,Ramphedi Mwasako.Wote hao kutoka ITV,
       
            Waraka huo uliwataja watangazaji wengine walionunuliwa kutoka Kituo cha Tv cha Chanel Ten ni David Ramadhani na katika Shirika la Utangazaji la Serika TBC ni Shabani Kissu.
    
             Pia Kituo cha Tv cha Star Tv ni Mzee Angalieni Mpendu na Francic Mawalla na waraka huo umeshindwa kuwataja watangazaji wa vituo vya ZBC pamoja Clauds Tv ambao wamenunuliwa ili kuipigia kampeni katiba iliyopendekezwa,
      

            Waraka huo ambao unasema kila mtangazaji atapewa Sh laki mbili kwa kila kipindi kitakachorushwa na wachambuzi ambao watakua wanachambu kataiba  watapewa laki tano kwa kila kipindi.

 Katibu Mkuu wa Chadema Dokta Slaa aliwataka watanzania kuvipuuza vipindi hivyo pamoja na watangazaji hao kwa mdai watakuwa wanafanya kazi tofauti na sheria za vyombo vya Habari.


No comments: