.

MAKUBWA YAANZA KUIBULIWA SAKATA LA MAKONDA,ELIMU YAKE KUMBE NI----SOMA HAPA

Na Karoli  Vinsent


HUKU ikiwa bado wasomi,wanasiasa na wanaharaki pamoja na taasisi mbalimbali zikiwa zinalaani vikali kitendo cha wahuni waliokodiwa na aliyekuwa Mjumbe wa Bunge Maalum la katiba Paul monda kuvuruga na kupigwa aliyekuwa 

            Mwenyekiti wa tume ya ukusanyaji Maoni ya Katiba mpya Jaji Joseph Warioba wakati mdahalo wa kutoa
  elimu kuhusu katiba iliyopendekezwa na Bunge maalum la katiba,sasa Mapya yaibuka kuhusu Fujo hizo,Mtandao huu unariboti

              Taarifa za kuaminika ambazo Mwandishi wa Mtandao huu amezipata zinasema Chama cha Mapinduzi CCM kilikuwa nyuma za vurugu hizo zilizoibuka wakati wa mdahalo huo wa kutoa elimu kuhusu katiba,na kiongozi wa vurugu hizo ametajwa kuwa ni Paul makonda katibu wa uhamisishaji wa umoja wa Vijana (UV-CCM),
          

  Chanzo hicho kinasema Makonda ambaye anadaiwa kukodisha vijana na kuwapa posho ili kuandika mabango ,kuyaingiza ukumbini na kutoa taarifa lini wanayanyue mabango yao  ili kupoteza Mwelekea ukumbini hapo,
           
  Na ndivyo ilivyotokea ukumbini hapo siku ya jumapili wakati wa kungamano hilo Ubungo Plaza Jijini Dar Es Salaam,
     
     Makonda ambaye nyaraka mbalimbali zinamuonyesha akitumia Jina Paulo Christian Makonda kutoka Wilayani Sumve,Mkoani Mwanza.
     
  Taarifa hizo kutoka  kwa watu waliokaribu na Makonda  zinasema kiongozi huyo wa UV-CCM alimlipa kila kijana aliyefanya vurugu kiasi cha sh 50,000(elfu Hamsini)
    
  Taarifa hiyo ilizidi kusema  mkutano wa Makonda kupanga njama za kuvuruga mdahalo huo,ulifanyika siku Jumamosi ambapo kabla ya siku moja kufanyika kwa mdahalo na mkutano huo ulifanyika katika Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam,
        
     Ambapo mbali na Makonda  kada mwingine aliyeshiriki katika uhuju hiyo alikuwa ni Salum Hapi ambaye ni katibu wa Zamani wa CCM katika vyuo vikuu vya Mashariki na pwani ambaye sasa yupo makao makuu ya UV-CCM akisubili kupewa uongozi.
       
  Makonda ambaye ni Kijana anayetumiwa na Msaka urais Samwel Sitta ,ndiye alikuwepo katika mipango ya  kuanzisha chama cha Jamii CCJ.
      
   Vyanzo mbalimbali vinamtaja Makonda ambaye alikuwa anatumwa na Samwel Sitta kwenda  kwa Dk Wilbroad Slaa,katibu mkuu wa Chadema katika mpango wake wakuhamia chama hicho kikubwa cha Upinzani nchini.
      
  Mtandao huu umedokezwa Jina la Christian ambalo Makonda anatumia  kwa miaka mingi sio la kwake halisi,inadaiwa  alijipachika jina hilo baada ya kufeli masomo yake  ya Sekondari.
      
   Ambapo Mwenye Jina hilo hasa ni Paul Christian ni Mwandishi wa Habari ambaye anafanya kazi redio ya Kijamii Mkoani Tabora.
          
  Ujumbe wa simu ulionaswa na Mtandao huu,unaonysha wazi kwamba Paul Makonda ndiye aliyepanga mikakati hiyo ya kuvuruga vurumai ukumbini hapo,

“Tuliitwa jana (Jumamosi)  na Makonda tukapewa malekezo kuwa twende Ubungo plaza kuvuruga mdahalo ,tulikuwa ma kikundi cha watu 25 hadi 30  ila leo tulifika watu 15 “ unaleza ujumbe mmoja wa simu
        
  Ujumbe huu mwengine  ulitumwa na kigogo wa chama cha Mapinduzi CCM  saa 11.39 jioni muda mfupi baada ya mdahalo kuhailishwa ulisema hivi

“Wengine hawakutokea kwasababu nadhani waliogopa ingawa posho ndogo walichukua,tulifika ukumbini wakati mdahalo ushaanza”
       
  Kwa Upande wake mwenyekiti wa Chama cha wananchi CUF  Profesa Ibahimu Lipumba alilani vikali uhuni huo aliofanya Makonda wakati wa Mkutano na Waandishi Wahabari juzi jijini Dar es Salaam,alisema kitendo alichofanya makonda kinafaa kulaniwa na kila mtu.

Nao Asasi mbalimbali za kiraia zimelaani vikali kitendo cha kipuuzi alichofanyiwa Jaji warioba, Akisoma tamko la asasi hizo za kiraia kwa waandishi wa habari juzi Jijini Dar es Salaam, Msomaji wa tamko hilo Bi Hellen Kijjo Bisimba Ameweka wazi kuwa tukio la kupigwa kwa warioba lilipangwa na genge la watu wachache ambao walikuwa na nia ovu ya kuharibu mkutano huo abao ulilenga kutoa elimu kwa wapiga kura,

        Aidha asasi hizo ambazo zilikuwa zikiongea kwa uchungu kutokana na kupigwa kwa Warioba, Wameionya vyombo vya dola kuhakikisha kuwa huo unakuwa ni mara ya mwanzo na ya mwisho kutokea kwa vurugu kama hizo kwani kitendo cha kuachilia hali kamahiyo kuendelea kutokea kutalipelekea taifa katika vita dhito amabayo itagharimu maisha ya awatanzania wote


About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.