Monday, November 17, 2014

HIVI NDIVYO VIJIWE VIKUU VYA WAUZA UNGA TANZANIA


SERIKALI YATAJA VIJIWE VYA WAUZA 'UNGA'
Serikali imetaja vijiwe vya wauzaji wa dawa za kulevya ‘unga’ vilivyopo katika mikoa mbalimbali nchini. Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu hali ya dawa za kulevya hapa nchini.

Lukuvi alisema dawa hizo hutumika zaidi kwenye vijiwe maarufu kama vile Ngarenaro na Mianzini mkoani Arusha, Msamvu (Morogoro), Hazina, Kituo Kikuu cha mabasi (Dodoma), Meko na Mbuyuni (Kilimanjaro). Vijiwe vingine ni Kirumba, Nyamagana na Mbita(Mwanza), Kwa Mama John, Mafiati na Mwanjelwa (Mbeya), Vigaeni, Sinani na kituo cha mabasi (Mtwara), Mwanga na Ujiji (Kigoma), Majengo, Kakora na Makaburini (Shinyanga), Mtego wa Simba (Kahama) na Sahare, Deep Sea, kituo cha basi, Barabara ya 11 na 12 katika Jiji la Tanga.

No comments: