“Dovutwa amesema vyama hivyo vimeamua kushirikiana kwa sababu vipo vyama vilivyounda kundi lisilokuwa la kisheria linaitwa Ukawa, lakini hakuna sheria inayoturuhusu kuunganisha vyama ila tunaweza kushirikiana tu ndiyo maana tunasema tumekubaliana kushirikiana”. vyama vilivyokubaliana kushirikiana ni SAUT, DEMOKRASIA MAKINI, JAHAZI ASILIA, UMD, UMD, UPDP NA AFP , Katika picha wanaofuatia ni Dominic Lyamchai Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia Makini, Rashid Lai Katibu Mkuu AFP na baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa.
Mwenyekiti wa Chama cha SAUT Yusuf Manyanga akifungua mkutano huo kabla ya Mwenyekiti wa UPDP Mh. Fahmi Dovutwa kutoa tamko.
Rashid Lai Katibu Mkuu AFP akifafanua jambo wakati wa mkutano huo uliofanyika Sinza jijini Dar es salaam kutoka kulia ni Mwenyekiti wa Chama cha SAUT Yusuf Manyanga , Mwenyekiti wa UPDP Mh. Fahmi Dovutwa na Dominic Lyamchai Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia Makini
No comments:
Post a Comment