Lori la ndizi ambalo limesheni likisubiri zamu yake kushusha katika soko la nadizi mabibo, soko hilo linaelezwa ndilo soko peke lenye mahakama yake, kwa habari kamili soma hapa |
Zamani si rahisi kukuta soko hili likiwa na bidhaa tofauti zaidi ya machungwa sasa ni kawaida baada ya genge la watu wachache kuona kuna mwanya wa kupiga pesa kirahisi |
UWAMANDIMA: CHAMA KINACHOTENGENEZA MABILIONI YA SHILINGI YANAYOINGIA MIFUKONI MWA WATU WACHACHE HUKU WAKULIMA WAKIZIDI KULIA NA KUSAGA MENO
Huku wakulima wakilia na kusaga meno kuhusu bei za pembejeo na gharama za usafirishaji zikiwa juu, imebainika katika masoko ambayo wanapeleka bidhaa zao kumekuwa na magenge ya watu wachache wanarudisha nyuma juhudi za rais na wakulima kwa ujumla katika kuinua sekta ya kilimo
Katika soko la mahakama ya ndizi jijini Dareslaam,ndilo soko pekee ambalo lilionekana kama mkombozi kwawakulima lakini ukweli ambao fullhabari umefunuriwa ni kwamba chama cha wafanyabiashara wa sokoni hapo limekuwa ni genge la kufadhili wezi, wa ndizi pamoja na ubadhirifu wa mamilioni ya shilingi
Sokoni hapo inaelezwa kunanuka Wizi, uonevu, ubadhirifu, ubabe na utembo ambalo kwa silimia kubwa umekuwa ukilindwa na chama cha wafanyabishara wa soko hilo wachache wanaojiita UWAMANDIMA
Sikumoja fullhabari kama kawaida yake ikiwa kazini ilipata simu ya dharula kutoka moja ya wafanyakazi wa sokoni hapo wakimtaka mwandishi wetu ende haraka sokoni hapo kuchukua habari,hakika mambo ambayo yameshuhudiwa nadiriki kusema soko hili huenda liko katka nchi ya angani ambayo rais wake hafamiki, hakuna mtu anayejali dhurma inayofanywa na watu wachache waliojingea utamaduni wa utembo ambao wapo kwa ajiri ya kumnyonyonya mkulima,
Kifupi soko la mahakama ya ndizi na madudu yake ni haya hapa
Soko la mahakama ya ndiz linasehemu tatu ambayo imegawanywa kutokana na bidhaa ambazo huuzwa ambapo kuna sector ya Nyanya, Mbogamboga na Ndizi. Na kila sehemu kuna uongozi wake ambazo kwa hakika kuna madudy ya aina yake ndani yake, Fullhabari leo hii imejikita dhaidi katika sekta ya ndizi ambayo ndiyo unyanyasaji mkubwa umeonekana kukithiri huku hakuna mtu wa kukomboa hali hiyo,
Upande huu wa Ndizi soko linaongozwa na chama kimoja maarufu sna wanakiita “UWAMANDIMA”chama hicho kinaongozwa na genge la watu 356 ambao hukutana mara mbili kwa mwaka na kugawana posho kubwakubwa kwa kila mmoja huku mkulima akibaki analia bila sabu yoyote,
MADAI YA WAKULIMA WA NDIZI SOKONI HAPO
Chama cha uwamandima kinauongozi wa wa aina yake sana, kuna watu wanajiita makamanda, wengine mabususu. Watu hawa wameonekana kuwa na madaraja tofauti ambao hunyonya mkulima kwa style ya aina yake,Leo hii nitakulezea kwa umakini kuhusu Mnyonyaji namba moja anaykusanya zaidi ya milioni saba kwa wiki bila kufanya kazi
MAKAMANDA
Hawa watu kwanza wako 60 tu soko zima ambao kazi yao kubwa haieleweki, watu hawa wamekuwa wakilelewa kwa muda mrefu na kula fedha za wakulima bure tena bila kuchafuka, inadaiwa kuwa watu hawa ndio wanaokula 20,000 ya kila gari inayoingia sokoni hapo,
Utafiti uliofanywa na fullhabari mpaka sasa, unaonyesha kuwa soko hilo la mahakama ya ndizi limeendelea kuwaheshimu watu hawa wanaokingiwa migongo na chama nyonyaji cha UWAMANDIMA ambao hawako tayari kuondoa genge hili la watu 60
Fedha zinazopotea kwenda kwa makamanda
Kwa siku jumla ya gari 30 zinaingia sokoni hapo ambapo kila gari ni lazima itoe jumla ya shilingi 20,000 kuwapa kamanda wa siku hiyo, na jioni ikifika kamanda anapitisha mchango kwa wafanyabiashara wote wa soko hilo kwa kigezo kuwa wanataka kuwalindia na kama hutaki kulipa ujue mzigo wako mali yao na soko hilo hutakiwi
Katika mchango huo, wafanya biashara wote wanalipa kati ya 400 hadi 2000 ili kulindiwa mzigo wako ambapo jumla ya pesa zote kwa siku anazokusanya kamanda wa siku husika ni kama Milioni na ushehe hivi,
Mpashaji habari anasema Makamanda huwa wanapeana zamu ambapo kila kamanda anafanya kazi kwa muda wa wiki moja na kumpisha mwenzake ambaye naye anakaa kwa muda huo hadi wote 60 wamalizike ndipo zamu inarud tena kwa kamanda wa zamu ya kwanza,
Hesabu zilizopigwa kwa wiki kamanda anaweka kibindoni jumla ya milioni saba (7,000,000) ambazo anaiba kutoka kwa mkulima mlala hoi,
Ukamanda unapatikana vipi
Mtoa habari anasema, si rahisi kuukwaa UKAMANDA katika soko la MAHAKAMA YA NDIZI, kuupata ukamanda ni sawa na kuuaga umaskini.
Kwanza ili uwe kamanda Ni lazima uwe mwanachama wa Uwaamandima, lakini napo si rahisi kuwa mwanachama wa uwamandima.
Watafiti wa soko hilo wanasema Ukamanda unarithisishwa kama ulivyo urithi mwingine wowote ama unaweza kuununua kama kuna mtu mmoja wapo toka kwenye genge la watu wachache hao kutaka kuuza jina lake,
Utafiti uliofanywa na fullhabari umebaini kuwa tayari kuna watu kadhaa na ushahidi tunao, wamesharithishwa ukamanda katika soko hilo na wanaendelea kupiga pesa tena bila kulipa kodi,
Wakati tukiendelea kulimulika soko hilo kwa siku za usoni tutawawaletea makala tosha ya kuelezea jinsi serikali inavyopoteza mabilini ya shilingi kutoka soko hili kubwa linalonyonya wakulima,
BEI YA UKAMANDA
Ukamanda unanunuliwa kwa jumla ya shilingi milioni tano 5,000,000, na kama hauna huwezi kuupata ukamanda, tena siyo kila mtu anaweza kununua ukamanda, ni lazima uwe mmoja wa genge la watu wa UWAMANDIMA ndipo uwe umekizi vigezo vya kupata ukamanda
Mabususu wao ni watwana wa MAKAMANDA ambao huwatumikisha kazi ngumu huku makanda wakila kuku kwa mrija
No comments:
Post a Comment