Naibu katibu mkuu wa chama hicho bara bi MAGDALENA SAKAYA akizngumza na wanahabari muda huu jijini dar es salaam |
Chama cha wananchi CUF kimesema patachimbika pamoja
na damu kumwagika endepo kama serikali itaendelea na vurugu na mchezo mchafu
unaochezwa katika maandalizi ya kuelekea chaguzi za serikali za mitaa
unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu.
Akizungumza na wanahabari muda huu jijini dare s salaam
naibu katibu mkuu wa chama hicho bara bi MAGDALENA SAKAYA chama chake
kinasikitishwa sana na jinsi ya serikali ya chama cha mapinduzi kuvuruga
uchaguzi wa serikali za mitaa kwa makusudi kwa kuandaa machafuko kwa kutunga
kanuni mbaya isiyotekelezeka kanuni mwongozo mbovu wa uchaguzi huo.
Amesema kuwa hii ni dalili kuwa serikali ya chama
cha mapinduzi ilikurupuka katika kuandaa
uchaguzi huo na haikuwa na mpango kamilifu wa kufanya uchaguzi huo ndani ya
kpindi hiki kama ambavyo kumekuwa na kauli zinazokinzana kati ya Rais KIKWETE
pamoja na waziri mkuu MIZENGO PINDA kuhusu tarehe za kufanyika uchaguzi huo.
Baadhi ya maneno ya kutisha yanayopatikana katika tamko la CUF LEO |
Akitaja mapungufu hayo ya uchaguzi huo ni pamoja na
kutoa mwongozo wa utekelezaji wa kanuni za uchaguzi ambapo maelezo yake
yanakinzana ambapo katika kanuni ibara ya 15 kifungu cha 1 kimejieleza vizuri
na kutoa fursa kwa mtiririko wa namna ya kuweka pingamizi hadi kujadiliwa kwa
rufaa na kila jambo limetengewa muda wake wa utekelezaji lakini katika mwongozo
mtoririko huo haupo badala yake unaelekeza maeneo mawili tu ambayo hayaendemio
sambamba muda wa kuwakilisha pingamizi kwa msimamizi msaidizi ambapo ni siku
nne na muda wa kamati ya rufaa kusikiliza rufaa ambapo ni siku nne na imetajana
tarehe zake za utekelezaji nov 26 hadi 29 lakini wakati huo huo hakuna muda wa
kusikiliza pingamizi hiyo kwa msimamizi msaidizi hakuna muda wa kukata rufaa
kama hujaridhika na maamuzi ya msimamizi msaidizi.
Wanahabari wakisikiliza kwa makini |
SAKAYA amesema kuwa malalalamiko hayo pamoja na
mengine mengi wamekwisha yafikisha katika ngazi husika na kamwe hawatakubali kuona
wanachezewa mchezo mchafu na kama serikli haitaacha mchezo huo patachimbika
No comments:
Post a Comment