Chama cha ushirika cha akiba na mikopo cha TCRA leo kimefanya mkutano wake mkuu wa pili wa wanachama wake ambapo pamoja na mambo mengine wameutumia mkutano huo kupata viongozi wapya wa chama ambao watakiongoza chama hicho kwa mhula mwingine wa uongozi. Mkutano huo uliofanyika mkao makuu ya mamlaka ya mawasiliano Tanzania umeshughudia wanachama hao wakipata viongozi wapya kama unavyowaona kwenye picha hapo.
Viongoi waliochaguliwa ni pamoja na mwenyekiti mpya ambaye amerudishiwa nafasi yake bw ERASMUS MBILINYI ,pamoja na makamu mwenyekiti MABEL MASASI,wengine ni wajumbe wapya wa bodi ya chama hicho ambao ni ABDULL HUSSEN,MASAI J MASAI,CHARLES THOMAS,BENJAMIN MWANDETE,na GABRIEL MRUMA. |
No comments:
Post a Comment